The House of Favourite Newspapers

KAJALA AITAMANI NDOA TENA!

ANA umbo kubwa lakini linalompendeza na kumwacha na mvuto wake wa kipekee. Staili yoyote ya nywele inamtoa chicha, kwenye mavazi ndiyo kabisaaa, kila anachotupia anatokelezea.

 

Ongea yake sasa ndiyo balaa! Lakini shepu yake inaweza kuwa ndiyo silaha yake kubwa zaidi kuliko zote, maana ni hatari asikuambie mtu.

Namzungumzia Kajala Masanja anayetesa kwenye tasnia ya filamu za Kibongo. Ameshiriki filamu nyingi ambazo amefanya vizuri, lakini Devil’s Kingdom aliyocheza na marehemu Steven Kanumba (RIP), Mnigeria Ramsey Nouah na mastaa wengine wa Bongo ilimuweka pazuri zaidi.

 

Kazi zake nyingine ni pamoja na Basilisa aliyoshiriki na mastaa wengine Issa Mussa ‘Cloud’, Single Mtambalike ‘Richie’, Adam Kuambiana (RIP), Suleiman Said ‘Barafu’, Wema Sepetu na Ummy Wenceslaus.

Ni mama wa mtoto mmoja, Paula aliyezaa na prodyuza maarufu nchini Paul Matthyess ‘P Funky’. Baada ya kuachana na P – Funk alifunga ndoa na Faraji Chambo, ambaye alikuwa gerezani lakini kwa sasa ameshatoka.

Kajala katika special interview na Risasi Jumamosi, amefunguka mengi, huku akieleza kuwa baada ya kukaa singo kwa muda mrefu, kwa sasa anatamani sana kuolewa.

 

Fuatilia interview nzima hapa chini;

Risasi Jumamosi: Kajala kwa siku za karibuni umekuwa huonekani ukijichanganya sana, kwa nini?

Kajala: Kuna wakati unafika unaacha mambo mengine. Mambo hayo niliyafanya miaka ya nyuma. Mimi sasa ni mtu mzima, mwanangu Paula yupo kidato cha sita, sidhani kama kuna starehe ambayo sijafanya.

 

Risasi Jumamosi: Ulishaolewa lakini mumeo alipata matatizo, hujawahi kuimbuka ndoa yako?

Kajala: Naikumbuka sana ndoa, naweza kusema kwa sasa nimekuwa mkubwa, najitambua, najielewa. Kwa kweli akitokea mwanaume yupo serious naolewa wakati wowote, maana sioni sababu ya kuchelewa tena.

Risasi Jumamosi: Mume wako Faraji ameshatoka jela, akitaka muendelee itakuwaje?

 

Kajala: Mh! Hilo sidhani kwa sababu mambo mengi yametokea, hata hivyo sijawahi kumuona tangu atoke gerezani. Lakini nadhani hata yeye atakuwa na uhusiano na mtu mwingine.

Risasi Jumamosi: Vipi kuhusu mtoto, maana Paula ameshakuwa mkubwa. Una mpango wa kumletea mdogo wake?

Kajala: Nitafanya hivyo hivi karibuni tu, maana natamani sana, sana, sana!

Risasi Jumamosi: Vipi kuhusu malezi ya mtoto na kumsomesha?

 

Kajala: Unajua mama siku zote anakomaa na mtoto wake, hivyo nitasimama na mwanangu mwanzo mwisho na baba yake (P Funk) akitaka kuendelea anakaribishwa.

Risasi Jumamosi: Mastaa wengi wanaingia kwenye vishawishi vya kujitumbukiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya, hujawahi kushawishika? Je, unatumia pombe?

 

Kajala: Kwa sasa hapana, lakini nakiri huko nyuma niliwahi kunywa pombe na kuvuta bangi, lakini kwa sasa sigusi chochote katika hivyo. Kama nilivyosema tangu mwanzo, mimi kwa sasa ni mtu mzima. Nimeachana na ujinga wote.

Risasi Jumamosi: Sanaa ndio kazi uliyoamua kufanya lakini naona kama umeipa kisogo na kugeukia mambo mengine. Vipi, kwa nini umeamua kufanya hivyo?

 

Kajala: Kazi ya sanaa ina changamoto nyingi sana, huwezi kusema kuwa unasubiria hela ya filamu ukatoka. Ni shida, hivyo niliamua kujichanganya na kutafuta kazi nyingine.

Risasi Jumamosi: Mastaa wengi hawapendi kufanya kazi kabisa, kwa nini wewe kwako limekuwa wazo jepesi?

Kajala: Hilo halihitaji hata ushauri wa mtu yeyote, lazima kufikiria mwenyewe maana maisha yako yapo mikononi mwako. Kwa hiyo nilitulia, nikatafakari kisha nikachukua hatua.

 

Risasi Jumamosi: Kutokana na kazi yako unayofanya sasa, unaweza kusema umefaidika na kitu gani?

Kajala: Nimevuna vingi kwa kweli na Mungu akipenda, nitafungua ofisi yangu kubwa. Kuna taratibu nazikamilisha tu.

Risasi Jumamosi: Mastaa wenzako wamekuwa watu wa kujichanganya na unakuwa unajua kabisa kuwa staa fulani, rafiki yake ni fulani. Mbona wewe kwa sasa kwenye mambo ya ushosti unaonekana kurudi nyuma?

 

Kajala: Nimegundua marafiki wengi wanarudisha maendeleo nyuma, mnakuwa hamuendelei zaidi ya starehe tu, ndiyo maana nimeamua kwa sasa kuachana na hayo mambo na kupambana zaidi na maisha maana ni magumu sana.

Risasi Jumamosi: Asante sana Kajala kwa ushirikiano wako.

Kajala: Asante sana nawe, karibu tena wakati mwingine.

MAKALA: Imelda Mtema

JPM AMWAGA AJIRA, AMPANDISHA CHEO KANALI KUWA BRIGEDIA

Comments are closed.