KAJALA AITIFUA NDOA YA P-FUNK

Kajala.

 

MAMBO ni moto! Staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja anadaiwa kuitifua vikali ndoa ya mzazi mwenzake, Paul Matthysse ‘P-Funk’ kwa madai kuwa, amerudisha majeshi kwa prodyuza huyo wa muziki wa Bongo Fleva.

 

Mtoa taarifa makini ameeleza kuwa, kwa sasa ndoa ya P-Funk imetifuka kwani mkewe aitwaye Samira amemjia juu mumewe kuhusu ishu yake ya kurudiana na Kajala kwani watu mbalimbali wamekuwa wakimpigia simu na kumweleza kwamba wamemuona mumewe huyo akiwa na Kajala.

 

“Ndoa ya P-Funk kwa sasa inawaka moto kwa kweli maana hakuna maelewano kabisa na mkewe ana mimba kubwa tu ya mtoto wa tatu na vurugu zote hizo zimesababishwa na Kajala ambaye anasemekana amerudiana na mzazi mwenzake huyo ambaye kabla ya kuachana walijaliwa kuzaa mtoto mmoja wa kike ambaye ni Paula,” alivujisha mchapo mtoa taarifa.

 

Licha ya chanzo kuzungumza hayo, katika mtandao wa kijamii wa Instagram hivi karibuni kulichafuka kutokana na mke wa P-Funk kutoa maneno makali ya jinsi anavyosumbuliwa na watu kuhusu mumewe kurudiana na Kajala ambapo aliandika pia kwamba P-Funk amwache atailea mimba mwenyewe kwa kuwa siyo ugonjwa.

P Funk.

 

Katika kurasa za umbea habari kubwa ilikuwa ni hiyo huku Kajala akitakiwa kuachana na P-Funk ili ndoa yake iwe na amani kuliko hivi sasa imetibuka huku mkewe akiwa ni mjamzito hivyo amhurumie mwanamke mwenzake huyo.

Ijumaa lilimtafuta Kajala ili kuzungumzia madai hayo ya kutibua ndoa ya P-Funk baada ya kurudiana naye kimapenzi ambapo alikuwa na haya ya kusema;

 

“Nashangaa kwa nini huyo mke wa P-Funk hajiamini wakati anatarajia kuzaa mtoto wa tatu sasa, mimi sijarudiana naye ila huyo ni mzazi mwenzangu tu, namsihi ajiamini maana huyo ni mume wake tu.”

 

Kwa upande wa mke wa P-Funk alipoulizwa alieleza; “Huyo Kajala kama yeye anajiamini sana kwa nini asiposti picha za huko anakoendaga na P-Funk kwenye Instagram…kwanza simfahamu muulizeni huyo P-Funk kuhusu hayo mambo yao.”

 

Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta P-Funk ili kuzungumzia suala hilo lakini simu yake ya mkononi iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

STORI: GLADNESS MALLYA NA IMELDA MTEMA

Loading...

Toa comment