Kajala Amepata Mrithi wa Harmonize

MWANAMAMA mwingine kunako Bongo Movies, Kajala Masanja ameibua maswali kwamba huwenda amepata mrithi wa aliyekuwa mpenzi wake ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Harmonize au Konde Boy Mjeshi.

Kajala anasema kuwa, ana furaha sana na mtu aliyenaye kwa sasa hivi maishani mwake. Pia Kajala anasema kuwa, ana furaha sana kwa watu ambao walimuacha na anawashukuru na kufurahia kwa kumuacha.

Kauli zake hizo ndizo zimeibua hisia kwamba inawezekana amepata mtu mpya na anaowashukuru labda ni Harmonize, Quick Rocka au Majani kwa kuondoka kwenye maisha yake kwa sababu hao ndiyo wanaojulikana zadi kwamba walishakuwa naye.

Katikati ya mwaka huu (2021), Kajala alitengana na mpenzi wake ambaye alikuwa ni Harmonize baada ya kuvuja ile video maarufu ya ‘washa taa’ iliyosekana jamaa huyo alikuwa anamtongoza mtoto wa Kajala, Paula Kajala ambaye kwa sasa ni mpenzi wa msanii wa Bongo Fleva, Rayvanny au Van Boy.

STORI; WAANDISHI WETU, DAR

4231
SWALI LA LEO
YANGA/SIMBA KIMATAIFA
Baada ya usajili wa nguvu, mechi za Siku ya Wananchi na Simba Day kisha mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Ngao ya Hisani, je, ni timu gani unaamini itafanya vizuri kimataifa?Toa comment