The House of Favourite Newspapers

Kajala amliza mumewe jela

0

kajalaStaa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’

Baada ya kuenea kwa madai kuwa staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ amepangishiwa bonge la mjengo na kigogo mmoja (jina kapuni), mumewe Faraji Agustino anadaiwa kulizwa na vitendo vya mkewe huyo vinavyomuumiza akiwa jela.

Mbali na kigogo huyo, pia mwanadada huyo anadaiwa kutoka kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Abbott Charles ‘Quick Rocka’, habari iliyoripotiwa na gazeti hili toleo lililopita ambayo nayo wambeya walimfikishia na kumfanya ajisikie vibaya.

KajalacropHarusiKajala na mumewe siku ya ndoa.

Habari kutoka kwa mmoja wa ndugu wa Faraji ambaye amekuwa akimtembelea jela kumjulia hali zilidai kwamba, Kajala amekuwa akimliza mwenza wake huyo kutokana na maneno ambayo amekuwa akipelekewa kuhusu tabia zake za sasa huko mtaani.

“Kuna siku Kajala alikwenda kumtembelea kule gerezani, Faraji akajisikia faraja sana na kuona kumbe mkewe bado anampenda na kumjali. Siku chache baadaye akapata taarifa kuwa, mkewe huyo anatoka na yule mwanamuziki sijui wanamuita Quick Rocka aliumia sana na kujikuta akitokwa na machozi,” alisema mtoa habari huyo.

rock
Quick Rocka.

Baada ya kupata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Kajala na kumuuliza juu ya madai hayo, alipopatikana alisema: “Kama mwezi mmoja hivi kabla ya kwenda mikoani kwenye hizi harakati (kampeni) za CCM (Chama Cha Mapinduzi) nilikwenda kumuona na kumjulia hali, yupo vizuri tu na wala hamna shida yoyote. Hayo ni maneno ya watu tu.”

Machi mwaka jana, Faraji alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela au faini ya zaidi ya Sh. milioni 200 baada ya kupatikana na hatia ya kutakatisha fedha haramu kwenye Benki ya NBC, Tawi la Dar ambapo alishindwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kujikuta ‘akiozea’ Gereza la Segerea hadi leo.

Katika msala huo uliomweka Faraji gerezani, Kajala alihukumiwa miaka mitano kwenda jela na mumewe huyo lakini mwanadada huyo alilipiwa faini ya Sh. milioni 13 na Wema Isaac Sepetu.

Leave A Reply