The House of Favourite Newspapers

Kajala anapata wapi jeuri hii?

0

c367kajala8891Imelda Mtema

FEDHA inaongea! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mwigizaji Kajala Masanja kupanga kwenye mjengo mpya wa maana na kuushehenesha samani na ‘vikorombwezo’ kibao hadi kufikia hatua ya watu kuhoji, amepata wapi jeuri hiyo ya fedha? Ijumaa limenasa mchapo kamili.

KAJALA (1)Kajala ambaye awali alikuwa akiishi maeneo ya Sinza-Madukani, kwa sasa amehamia katika mjengo huo mpya uliopo maeneo ya Mwenge jijini Dar.

KAJALA (2)Kwa mujibu wa chanzo, ndani ya mjengo huo, Kajala anaishi na mwanaye Paula huku akiwa amewaajiri wafanyakazi wa ndani watatu na kulindwa na kampuni maalum ya ulinzi.

KAJALA (3)“Yani Kajala ananuka hela. Mjengo wake mpya una kila kitu ndani. Ukiingia unaweza kupagawa kutokana na vitu vilivyomo ndani. Watu tunajiuliza ni nani anayempa jeuri hii maana filamu pekee haziwezi kufanya matusi haya,” kilisema chanzo hicho.

KAJALA (4)Baada ya kupenyezewa ‘ubuyu’ huo, mwanahabari wetu alitia timu nyumbani hapo kwa Kajala na kujionea nyumba hiyo ya kifahari aliyopanga sambamba na ‘mazagazaga’ kibao ya thamani yaliyomo ndani.

KAJALA (5)Alipoulizwa amepata wapi jeuri ya kupanga nyumba hiyo ya gharama ambayo hakutaka kutaja bei ya kodi, kuajiri wafanyakazi watatu na kampuni ya ulinzi, Kajala alidai mambo yote hayo ameyafanikisha kwa kazi ya mikono yake na si vinginevyo.

KAJALA (7)
“Unajua kuna kipindi cha nyuma nilitengeneza filamu zangu kama tano na nilikuwa na maana hata kama nisingepata zile hela kwa wakati ule lakini nilijua baadaye nitapata hela nzuri na nitatengeneza maisha yangu hivyo sasa ndiyo nimevuna matunda ya sinema hizo na kufanya haya unayoyaona,” alisema Kajala licha ya nyuma ya pazia kuwepo na madai kuwa kuna kigogo anamuweka mjini.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWSglobalbreakingnews.JPG

 

Leave A Reply