Kajala: kwani kuvaa kibukta kuna shida?
MWIGIZAJI mwenye umbo matata Bongo, Kajala Masanja amewashangaa mashabiki wake waliokuwa wakichonga kuhusu kibukta alichovaa, amesema kwani kuna shida gani na mbona watu wanapenda kudili na vitu vidogo? Kajala amechonga na Gazeti la IJUMAA kuwa kuvaa kibukta kwake siyo ishu ya ajabu kwa sababu yeye anavaa nguo za kila aina hasa za Kizungu, hivyo wasiumize vichwa.
“Kwani kuvaa kibukta kuna shida? Kuna vitu vingi vya kufikirisha watu. Siyo ishu ya watu kutumia muda wao kufikiria, kwani hayo ni mambo madogo sana,” amesema Kajala ambaye picha yake aliyopiga amevaa kibukta kifupi ilizua gumzo kubwa kwenye Instagram.
Stori: Imelda Mtema, Dar


