The House of Favourite Newspapers

KAJALA: NIKIPATA MWANAUME MKWELI NAOLEWA TENA !

Kajala Masanja

Mwan­amama mkali wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja ameibuka na kudai kuwa akipata mwanaume mkweli, mwenye upendo ataolewa kwa mara ya pili. Kajala aliliambia Risasi Jumamosi kuwa yeye kama mwan­amke bado anatam­ani kuingia kwenye ndoa na akitokea mwanaume mwenye mapenzi ya dhati ataolewa kwa mara ya pili.

“Nilishaolewa mara ya kwanza, la­kini kama mwanam­ke bado ninahitaji kuolewa, suala hilo lipo akilini kwangu, akitokea tu mwa­naume mkweli, naolewa,” alisema Kajala. Kajala aliolewa ndoa ya kwanza na mumewe Faraji Chambo ambaye alitenga­na naye baada ya kupata matatizo yaliyo­sababi­sha wao kuhu­kumiwa kufungwa jela. 

STORI:Imelda Mtema, Dar

Comments are closed.