Kajala, Quick Rocka penzi zito

Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja na staa wa Bongo Fleva, Abbott Charles ‘Quick Rocka’.

KWELI penzi ni kikohozi! Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja na staa wa Bongo Fleva, Abbott Charles ‘Quick Rocka’ wamedaiwa kuzama kwenye penzi zito licha ya wenyewe kutotaka watu wajue.

Madai ya penzi hilo motomoto yameshereheshwa zaidi baada Quick kutupia picha kwenye mtandao wa Instagram inayomuonesha akiwa amejichora ‘tatoo’ kifuani yenye jina la Kajala na kuzua maswali mengi kwa mashabiki wao.

Mwanamuziki huyo alitupia picha hiyo huku akielezea kuhusu ‘shoo’ yake anayotarajia kuifanya kesho Jumamosi katika Jiji la Mbeya ambapo watu wakaacha kuchangia kuhusu shoo hiyo, wakaanza kufurahia uhusiano wake na Kajala.

Baada ya kuinyaka picha hiyo huku vyanzo mbalimbali vikieleza wawili hao ni wapenzi, mwanahabari wetu alimtafuta Quick ili aweze kueleza kama wameamua kuweka mambo hadharani kwa staili ya mtandao, alipopatikana, alifunguka:

“Mimi mwilini nimemchora mama yangu kwa sababu nilikuwa nampenda na kumthamini sana na kwa Kajala ni mtu ambaye nakubali kazi zake na kile anachofanya na ni watu ambao pia tunashirikiana kwa kazi mbalimbali za sanaa ndiyo maana nimechora jina lake,” alisema Quick.

Kwa upande wake Kajala, alipoulizwa kuhusiana na kuchorwa jina lake kifuani na kuweka wazi kama wana uhusiano wa kimapenzi na Quick, alisema hapendi kuzungumzia suala hilo.“Mimi nisingependa kuzungumzia chochote kuhusu hiyo ishu maana wajuaji wameshaongea mengi,” alisema Kajala.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

Loading...

Toa comment