KAJALA: REDE ILINIFANYA NIPIGWE KILA SIKU

STAA wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja ameweka wazi siri yake ambayo hajawahi kuitoa na kudai kuwa alipokuwa mdogo alikuwa akichapwa sana na wazazi wake kwa sababu ya kuhusudu mchezo wa rede.

 

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Kajala alisema alitokea kuupenda kupitiliza mchezo huo kitendo kilichokuwa kikisababisha akitoka shule anavua nguo na kwenda kucheza na kusahau hata kula.

 

“Jamani rede ilikuwa kama nimechanjiwa kabisa maana kuna wakati hata nikiwa darasani nawaza nitatoka saa ngapi, tunakutanaga watoto wengi sana hivyo nacheza mpaka najisahau kabisa kama kuna kurudi nyumbani, kitendo kilichokuwa kikimkera sana mama yangu,” alisema Kajala

 

Staa huyo aliongeza kuwa kuna siku alitoka shule akaenda kucheza rede na nguo za shule na alijisahau mpaka saa mbili usiku, aliporudi tu alikuta katayarishiwa fimbo mzigo, akatandikwa na kuanzia siku hiyo alijikuta anauchukia mchezo wenyewe.

Stori: Hamida Hassan

 


Loading...

Toa comment