KAJALA SASA AUCHUKIA MWILI WAKE

Kajala Masanja

MREMBO kutoka Bongo Movies, Kajala Masanja amefunguka kuwa kati ya vitu ambavyo anavichukia kwa sasa ni pamoja na mwili wake kuwa mnene kupitiliza.

Ame-sema ubonge wake kwa sasa umefikia kiasi cha kumnyima raha kwani hata nguo zake nyingi ameshi-ndwa kuzivaa kwa sababu hazimpiti mwilini.

“Jamani huu mwili mpaka nahofia naweza kupata presha au gonjwa lolote linalotokana na kunenepa sana maana hata mazoezi naona sasa yamedunda, najitahidi kupambana ili niweze kurudi kama zamani,” alisema.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment