The House of Favourite Newspapers

Kajala: Sitamsahau Wema Hadi Kaburini

0

DAR: Staa mwenye viwango vyake kunako Bongo Movies; Kajala Masanja, ametamka waziwazi kuwa; “Sitamsahau Wema hadi nakufa!”

Kajala ameamua kuweka wazi juu ya mapenzi yake makubwa kwa mwanadada mwenye nyota zake kwenye Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ambaye alikuwa shosti wake mkubwa kabla ya kugombana.

 

Mwanamama huyo ameliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, kamwe hawezi kumsahau Wema hadi anaingia kaburini.

Kajala anasema kuwa, anajua bado Wema ana kinyongo kikubwa kwake kiasi cha kuweka wazi kwenye kipindi chake cha Cook With Wema Sepetu.

 

Anasema kuwa, kutokana na kinyongo, hawezi kuzungumza naye wala kuwa rafiki yake tena hadi anaingia kaburini.

“Mimi najua wazi Wema ana umuhimu gani kwenye maisha yangu. Kwanza mimi sina kinyongo naye kabisa na hata ikitokea naanguka (kufa) ghafla, bado Wema, atakuwa ni mtu wangu muhimu sana kwenye maisha yangu,” anasema Kajala.

Anaendelea kusema kuwa, anajua wazi Wema anaongea kwa hasira, lakini hafikirii kama ni kweli siyo mtu wa kusamehe.

Kajala anasema anachokifanya ni kuendelea kumuombea aondoe kinyongo kwenye moyo wake.

“Mimi kazi yangu ni kumuombea sana Wema, Mungu atamsimamia na kinyongo chake kitaisha kabisa kwa sababu mimi simchukii kabisa na ninampenda sana,” anasema Kajala akisisitiza hawezi kumsahau Wema maishani mwake.

 

Kajala na Wema waliingia kwenye bifu kali yapata miaka sita sasa kutokana na Kajala kuchepuka na aliyekuwa mpenzi wa Wema, Clement Kyondo ‘Ck’ na kuzuka mtafaruku mkubwa mkali sana kati yao.

Kabla ya ugomvi huo, Wema alimtolea Kajala faini ya shilingi milioni 13 na kumuepusha na kifungo baada ya kupatikana na hatia katika kesi ya utakatishaji pesa ya mwaka 2013.

Stori: Imelda Mtema, Ijumaa

Leave A Reply