Kartra

Kaka wa 21 Savage Adaiwa Kuuawa kwa Kuchomwa Kisu

KAKA wa rapa maarufu nchini Marekani, ShĂ©yaa Bin Abraham-Joseph ’21 Savage’, aitwaye Terrell Davis ameuawa kwa kuchomwa kisu jijini London.

 

Davis mwenye umri wa miaka 27 alichomwa kisu hadi kufa kufuatia majibizano na rafiki yake juzi Jumapili (Novemba 22) umeripoti mtandao Daily Mail.

 

21 Savage amethibitisha taarifa hizo kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram: “Nashindwa kuamini kama kuna mtu amechukua uhai wako kaka yangu, najua nimechukua hasira zako natamani ningerudisha muda,” aliandika 21 Savage.


Toa comment