The House of Favourite Newspapers

Kakolanya Apania Kuwaonyesha Yanga Taifa

KWA jinsi Beno Kakolanya alivyoipania Azam, Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Yanga lazima udenda uwatoke. Simba na Azam FC zitacheza kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ambao msimu uliopita Simba ilibeba ngao hiyo baada ya kuifunga Mtibwa Sugar.

 

Kakolanya ambaye ni kipa wa zamani wa Yanga, kwa mara ya kwanza tangu asajiliwe Simba ukiacha na mechi za kirafi ki alisimama kwa mara ya kwanza kwenye mechi ya mashindano pale Simba ilipoivaa UD Songo Jumamosi iliyopita nchini Msumbiji na kutoa suluhu.

 

Kipa huyo alidaka kwa mara ya kwanza huku kipa namba moja Aishi Manula alitupwa nje kutokana na kuwa majeruhi hivyo Beno alidaka akisaidiana na Ally Salim.

Akizungumza na Spoti Xtra, kipa huyo alisema maandalizi yao yanakwenda vizuri na kila kitu kipo sawa na lengo ni wao kuondoka na ushindi.

 

“Tunashukuru Mungu maandalizi yetu yako vizuri na tunaendelea na lengo letu ni kuona tunafanya vizuri kwenye mchezo huo, japo wapinzani wetu nao wamejipanga na wanahitaji kile ambacho na sisi tunataka.”

 

Kakolanya alisajiliwa na Simba kutokea Yanga kipindi cha usajili mkubwa baada ya kuvurugana na Zahera kutokana na kipa huyo kudai chake jambo ambalo lilimfanya asitishe mkataba wake ndani ya Yanga.

Comments are closed.