The House of Favourite Newspapers

Kakolanya auwasha moto Yanga SC

KIPA namba moja wa Yanga msimu huu, Beno Kakolanya amewataka wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuwa watulivu na kutoumizwa na matokeo ambayo waliyapata hivi karibuni dhidi ya Ndanda FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Kakolanya ambaye anashikilia rekodi ya kufungwa mabao mawili katika mechi tisa za Ligi Kuu Bara ambazo ameitumikia Yanga amesema kuwa kuanzia sasa hayupo tayari tena kuona nyavu zake zikitikisika.

 

Akuzungumza na Championi Jumatano, Kakolanya alisema baadhi ya mashabiki wa timu hiyo wameonekana kuvunjika moyo kutokana na matokeo sare ya bao 1-1 ambayo Yanga iliyapata hivi karibuni dhidi ya Ndanda FC na kuanza kuhisi kuwa tayari wameanza kutoka katika mbio za kuwania ubingwa jambo ambalo siyo kweli.

 

“Niwaambie tu kuwa bado mechi ni nyingi na waendelee kuwa na imani na timu yao, naamini kuwa tutaendelea kufanya vizuri kwani sisi na Azam pekee ndiyo timu ambazo hatujapoteza mchezo hata mmoja.

 

“Niwahakikishie kuwa wachezaji wote tupo sawa na tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri, hata hivyo kwa upande wangu nitaendelea kupambana kwa nguvu zangu zote ili kuhakikisha kuwa hakuna bao lolote litakalopita langoni kwangu,” alisema Kakolanya

Sweetbert Lukonge, Dar es Salaam

Comments are closed.