Kakolanya: Nikipangwa leo, Simba Hawatajuta

KIPA namba mbili wa Simba, Beno Kakolanya, amesema kuwa kama atapewa nafasi ya kuanza katika kikosi cha leo Jumatatu kitakachopambana na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi, anaamini kuwa hakuna watakachojutia wapenzi na mashabiki wa timu hiyo.

 

Simba itapambana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa fainali utakaochezwa leo kwenye Uwanja wa Amaan mjini Unguja, Zanzibar.

 

Akizungumumza na Championi Jumatatu, Kakolanya alisema kuwa yupo fiti na tayari kwa mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na historia iliyopo baina ya timu hizo kila zinapokutana katika michuano hiyo.

 

Hii ni mara ya tatu Simba kupambana na Mtibwa Sugar katika hatua ya fainali ya michuano hiyo ambayo huzikutanisha timu kutoka Zanzibar na Bara. Na mara mbili zilizopita 2008 na 2015, Simba ilishinda.

 

“Nipo vizuri kabisa kwa ajili ya mechi hiyo, lakini mpaka sasa sijui kama nitacheza au laa, lakini ikitokea nikapata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza, naamini nitafanya vizuri.

 

“Najiamini na wala sina wasiwasi wowote hivyo ni matumaini yangu pia hakuna watakachojutia wapenzi na mashabiki wa timu yetu,” alisema Kakolanya.

 

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam


Loading...

Toa comment