The House of Favourite Newspapers

KALA JEREMIAH AFUNGUKIA BIFU NA ROMA MKATOLIKI

Kala Jeremiah

MWANAMUZIKI Kala Jeremiah, ni zao la mashindano ya vipaji yaliyojinyakulia umaarufu mkubwa nchini yakijulikana kwa jina la Bongo Star Search.

Wimbo uliomtambulisha kwenye gemu la Hip Hop Bongo unaitwa Wimbo wa Taifa aliofanya na mwanamuziki Nakaya Sumari, lakini pia amefanya mambo mengine makubwa kwenye muziki nchini ukiachana na kutoa nyimbo kali zikiwemo Dear Lord na Wanandoto!

 

Kala ameweza kufanikiwa kuvuna kwenye muziki tuzo tatu kutoka Kilimanjaro Music Awards, ana tuzo moja ya Global Publishers, lakini pia ana cheti kimoja cha heshima alichopewa na taasisi iitwayo Society Watch, kutokana na wimbo uitwao Wanandoto, taasisi hiyo ikimtambua kama mwanamuziki anayefanya nyimbo zenye kuigusa jamii.

 

Ulipita muda, mkali huyu akiwa kimya, lakini hivi karibuni ameibuka kwa kuachia wimbo uliomrudisha ‘again’ kwenye ‘main stream’ uitwao Natabiri akiwa na mwanamuziki Water Chilambo. Over Ze Weekend limeweza kumnasa na kufanya naye mahojiano. Bonyeza hapa chini!

 

Over Ze Weekend: Hongera kwa kazi yako mpya, ni nzuri! Unaona imepokelewaje?

Kala: Kiukweli kazi imepokelewa vizuri kuliko hata mategemeo. Nilikuwa ninafahamu itapokelewa vizuri. Pia imekuwa zaidi ya nilivyokuwa ninawaza. Wimbo huu kwangu ni wa kwanza kupata ‘views’ zaidi ya laki moja katika muda mfupi kwenye Mtandao wa YouTube.

 

Over Ze Weekend: Umekuwa na kawaida ya kufanya kazi kisha unapotea, Kwa nini unafanya hivyo?

Kala: Unajua nyimbo zangu nyingi nimekuwa nikiimba ujumbe, kwa hiyo huwa inanibidi niache ujumbe ufanye kazi na ufike sehemu fulani kwa vijana, alafu ikifika hatua naona ujumbe huo umepenya ndiyo kama hivyo narudi tena.

 

Over Ze Weekend: Kuna stori kwamba kwa wanamuziki wanaoimba muziki wa aina yako wanabaki nyuma kwenye suala zima la mafanikio, kwani ni nje ya biashara ya muziki, stori hizi kwako ‘zina-make sense?

Kala: Kiukweli stori hizo nimekuwa nikizisikia na kuzisoma kwenye media, lakini ukweli ni imani potofu, biashara ya muziki haitegemei aina fulani ya muziki ambayo mtu anafanya. Ni mipango ambayo mtu anakuwa nayo kuifikisha kazi yake kwenye jamii na ieleweke.

 

Ndiyo maana hata hao wanamuziki wanaodaiwa kuimba nyimbo za biashara wanakuwa na menejimenti ili kusukuma kazi zao, sasa kama muziki wao unajiuza zaidi, kwa nini wasi-push bila kuwa na menejimenti? Kwa hiyo unaweza kuona muziki wa aina yoyote unaweza kuufanyia biashara.

 

Over Ze Weekend: Kwenye wimbo wako huu mpya, unapoanza tu unajitambulisha kama Nabii Yeremiah, ndiyo ‘a.k.a’ yako mpya?

Kala: Ni kama hivyo, unajua Yeremiah, kwenye maandiko ni miongoni mwa manabii waliofanya vitu vikubwa sana. Ukitazama hata kwa upande wangu kuna mambo makubwa ninafanya kwenye muziki ambayo wengi wameshindwa kufanya, kwa hiyo mtu hawezi kushitakiwa kwa kuniita Nabii Yeremiah!

 

Over Ze Weekend: Unaamini ‘views’ za Youtube ni kipimo cha kuonesha namna ambavyo kazi imekubalika?

Kala: Hapana, mwanamuziki ana watu wengi wa kuwafikishia ujumbe na kuipokea kazi yake. Siyo hao kwenye mitandao tu, mimi naamini kazi ikipokelewa vizuri na media iende sambamba na mtaani.

 

Over Ze Weekend: Unawaza kufanya kolabo na wanamuziki wa nje pia ili kutanua wigo wa mashabiki wako?

Kala: Ni kweli. Mipango ipo, ukitazama mimi ni muumini wa kolabo, nyimbo zangu nyingi ninafanya kwa kushirikiana, kwa hiyo ni mambo ya muda na Mungu akijalia, basi nitafanya kolabo pia na wanamuziki wa nje tena wenye majina makubwa, kwani kila kitu kinawezekana.

 

Over Ze Weekend: Una bifu na mwanamuziki Ibrahim Mussa ‘R.O.M.A?’

Kala: Hapana. R.O.M.A kwangu ni kama ndugu na hatuna tofauti zozote zile na sina background hasa ishu hiyo iliibukia wapi.

Over Ze Weekend: Lakini stori za ninyi kuwa na bifu zipo na ndiyo maana hampeani sapoti hata kwenye mitandao ya kijamii wala kuambatana kama zamani?

 

Kala: Niamini mimi hatuna bifu. Kwanza R.O.M.A kwa sasa ana kundi, kwa hiyo muda mwingi unakuta anafanya mambo yake na kundi lake. Hatuambatani tena ni kama ambavyo unaweza usimuone R.O.M.A na ndugu yake yeyote wakimbatana, lakini ukamuona na Stamina. Utasema haelewani na ndugu zake? Kuna muda tunaonana na mambo mengine yanaendelea, lakini si kwamba tuna tofauti. Kuhusu mitandaoni, ukitazama Instagram, kwanza ni kama hayupo vile, kwa hiyo tupo sawa.

 

Over Ze Weekend: Kwa hiyo hizi stori kwamba bifu lenu limesaba-bishwa na Dayna Nyange unathibitisha si za kweli?

Kalah: Ha! Ha! Haa! Aisee sikutegemea kabisa hili. Sema nikwambie ukweli, hizi ni stori za kupikwa tu, lakini sisi tupo sawa na uhusiano wetu ni kama familia.

 

Over Ze Weekend: Sawa, tumeona pia mastaa wakivuta majiko na kuoa, vipi kwa upande wako?

Kala: Kwangu kuoa ni ibada. Kwa hiyo muda ukifika ambao Mungu amenipangia nikamilishe ibada hii, basi nitakamilisha.

Over Ze Weekend: Tutegemee nini zaidi baada ya ujio huu?

Kala: Kwanza kwa sasa acha niisukume kazi hii, alafu mambo mazuri hapo baadaye yatafu

BONIPHACE NGUMIJE

Comments are closed.