visa

Kala Jeremiah: Nimeenzi lugha ya Kiswahili kwa ‘Wana Ndoto’

Kala Jeremiah Global (1)

Msanii wa Hip Hop, Kala Jeremiah akiwa Global TV Online siku ya jana. 

Kala Jeremiah Global (3)

Mhariri wa Ijumaa Wikienda, Sifael Paul (kushoto) akiwa katika pozi na Kala Jeremiah.

Kala Jeremiah Global (5)

Wafanyakazi wa Global Publishers, Nyemo Chilongani (kushoto) na Andrew Calos (kulia) wakifanya yao na Kala Jeremiah.

Kala Jeremiah Global (7)

Mhariri wa Championi Ijumaa, John Joseph (kulia) akiwa na Kala Jeremiah.

Kala Jeremiah Global (8)

Clarence Mulisa akiwa rafiki yake wa siku nyingi Kala Jeremiah.

Kala Jeremiah Global (9)

Mtangazaji wa  Global Tv Online, Kelvin Shayo (kushoto) akifanya yake.

Kala Jeremiah Global (10)

Mpiga picha wa Global Tv Online, Hihlali Daudi (kushoto) akiongea jambo na Kala Jeremiah.

Kala Jeremiah Global (11)

Video Editor wa Global TV, Shaban Juma (kushoto) akiwa na Kala Jeremiah.

MSANII wa Hip Hop, Kala Jeremiah akiwa Global TV Online alisema yeye ni mtetezi na mpigaji wa watoto yatima, kwani kile wanachokipata siyo mahitaji yao halisi.
“Watoto yatima waliopo katika makambi, wanachokipata ni kula, kulala na chakula, wanaohusika na watoto hawana lolote wanalojali zaidi kuwahusu, wanajadili mambo ya watoto kwenye makaratasi, kompyuta wakiwa kwenye viyoyozi, hawa viumbe wana mahitaji mengi zaidi ya hayo.
“Wanaohusika na watoto ni kama wamewatelekeza, mimi nimeshiriki na kuona matamasha mengi, yanayohusu Ukimwi na vitu vingine, lakini sijawahi kuona tamasha la watoto yatima, ndiyo maana nikatoa wimbo huu wa Wana Ndoto, kwa sababu na wao wana malengo wanayotaka kuyafikia, lakini hawapewi sapoti inayotakiwa.”
Kuhusu namna anavyoienzi lugha ya Kiswahili, alisema kwa kuanzia, aliamua kushughulika na jina la mtoto wake, kwani wazazi wengi wa Kitanzania wanawapa watoto wao majina yenye asili ya kizungu na kiarabu, yeye ameamua kumpa mtoto wake wa kwanza jina la Alama.
“Huyu akikua, akienda nje ya nchi, wenzake watamuuliza hili jina lako lina maana gani, atakapowaambia, utakuwa ndiyo mwanzo wa kukikuza Kiswahili, hili ndilo tunalotakiwa kulifanya wazazi wote, ni wajibu wetu kuhakikisha asili yetu haipotei,” alisema.   
(Habari na Abraham Ojukwu/GPL)Toa comment