Kalugendo na Mwenzake Wapandishwa Kisutu

 

MAPEMA leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Upande wa utetezi katika kesi inayomkabili Aliyekuwa Mkurugenzi wa Uthaminishaji Almasi na Vito Tanzania  (Tansort), Archard Alphonce Kalugendo na mwenzake umedai kuwa wateja wake wapo ndani kwa zaidi ya miaka miwili na upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.

 

Wakili wa utetezi, Nehemia Nkoko amedai kuwa  sasa ni miaka miwili imepita upande wa mashtaka unadai kuwa upelelezi haujakamikika jambo ambalo haliwezekani kila shauri hilo linapokuja  kauli iwe hiyo.

 

Akiiambia mahakama Wakili wa Serikali, Aldof Lema, amedai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo anaiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine ya kutajwa

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ameahirisha shauri hilo hadi Novemba Mosi mwaka huu.

Mbali na Kalugendo wengine ni Mthamini wa Madini ya Almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu, ambao ni watumishi kutoka wizara ya madini.

 

Kwa pamoja washitakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababisha serikali hasara ya zaidi ya Sh. bilioni 2.4.

Inadaiwa kuwa kati ya Agosti 25 na 31, 2017 katika maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam na Shinyanga, kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathamini walioajiriwa na Wizara ya Nishati na Madini waliisababisha serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha.

Toa comment