KAMA HUTAKI KUPATA MIMBA; FANYA HAYA

SAFU yetu wiki hii imebeba njia mbalimbali ambazo mwanamke anaweza kutumia ili asipate mimba kama hataki kuwa mjamzito.  Kutokujamiiana ndiyo chaguo mojawapo! Kama hutaki kupata mimba uamuzi sahihi na salama ni kuacha kujamiiana hadi pale utakapoamua kupata mimba.

UZAZI WA MPANGO

Njia nyingine ya kutopata mimba iwapo umeamua kuacha kujamiiana, uamuzi sahihi nikutumia njia za uzazi wa mpango. Njia mbalimbali za uzazi wa mpango zipo nenda kwa muhudumu wa afya atakuelekeza. Daima kumbuka kwamba ni kondomu tu inayoweza kukukinga na mimba na maambukizo ya magonjwa yatokanayo na kujamiiana pamoja Virusi vya ukimwi na ukimwi

Iwapo utachukua tahadhari ya kuepesha majimaji ya mwilini (damu, majimaji ya ukeni na mbegu za kiume ) yasingie/ yasiguse ukeni, kwenye uume, mdomoni au kwenye vidonda vilivyo wazi, unaweza pia kujikinga na virusi vya Ukimwi na magonjwa yatokanayo na kujamiiana.

Mwanamke yuko katika hali ya kupata mimba (kushika ujauzito) katika siku chache za kupevuka kwa yai kila mwezi ya mzunguko wa hedhi. Kuna njia za kutambua siku za kuweza kushika ujauzito na siku ambazo si za kushika ujauzito katika mzunguko wako wa hedhi. Zifahamu. Iwapo utafanya tendo la kujamiiana siku zile tu ambazo yai halijapevuka, una nafasi nzuri ya kutokupata mimba. Hata hivyo, sio rahisi kutambua ni siku zipi unazoweza kupata mimba, kwa kuhesabu.

Kuhesabu siku tu, kwa mfano kujamiiana katika wiki ya kwanza na ya mwisho ya mzunguko wa hedhi ya mwanamke (au ukikaribia siku za hedhi kutoka/siku zake) siyo njia salama sana.

Upimaji joto la mwili kila asubuhi kabla ya kuamka na kujiangalia utokaji/kudadisi aina ya ute kwenye uke kunaweza kukupa habari zaidi. Ingawaje njia hizi zinahitaji maelekezo na kujifunza kwa uangalifu ili zifanye kazi sawasawa. Kuacha kujamiiana kwa siku chache hakukukingi wewe na maambukizo ya magonjwa yatokanayo na kujamiiana pamoja na Virusi vya Ukimwi (VVU) na ukimwi.

Iwapo mwanamke atakukubaliana na mwanaume kumwaga mbegu za kiume nje, kunakuwa hakuna uwezakano wa kupata mimba. Hata hivyo, mbinu hii siyo salama kabisa na inatakiwa itumike tu katika mazingira ya dharura iwapo wapenzi wawili wameshindwa kabisa kutumia njia nyingine ya uzazi wa mpango. Kama mwenzi wako anakushauri njia hii, jadiliana kuwa kutumia kondomu kutakuwa na usalama kwenu na wote mtafurahia tendo. Pia hii siyo njia ya kumwaga mbegu nje si ya kutegemea kwa kujikinga na maambukizi ya magonjwa yatokanayo na kujamiiana.

KONDOMU CHAGUA SALAMA

Njia iliyo nzuri ya kuepuka mimba ambayo inashauriwa hata na Wizara ya Afya ni kutumia kondomu, njia hii ni ya uhakika na huzuia mimba zisizotakiwa na maambukizo ya magonjwa yaenezwayo kwa njia ya kujamiiana pamoja na Virusi vya Ukimwi (VVU) na ukimwi. Kuna kondomu za kike na za kiume.

VIDONGE VYA KUZUIA MIMBA

Vidonge vya uzazi wa mpango vya kumeza pia huwezesha mwanamke kutopata mimba. Vidonge hivyo ni lazima vimezwe kila siku bila kujali kama siku hiy mwanamke huyo atajamiiana au la. Kuna njia ya kuzuia mimba kwa mwanamke kuchomwa sindano maalum kila baada ya miezi mitatu, ieleweke kwamba njia hii haizuii maambukizi ya ukimwi au magonjwa mengine ya zinaa.

USHAURI

Ni jukumu la kila mmoja kuamua njia ambayo anaona inafaa kutumia katika kuzuia mimba zisizotakiwa. Ni vema kufuata njia hizi kuliko njia ambazo wanatumia wanawake wengine ya kutoa mimba baada ya kuingia. Kutoa mimba ni hatari tena ni kosa la jinai. Ukigundulika unaweza kufungwa jela. Kwa ushuri zaidi, wasiliana nasi kwa njia ya simu hii hapa kwenye safu.

Na mtaalam wetu, A.Mandai

Loading...

Toa comment