The House of Favourite Newspapers

Kama Kweli Anataka Kusepa… Rayvanny Achague Kuwa Harmonize Au Mavoko!

0

 

 

Mkali Wa Bongo Fleva Anayetumikia Lebo Ya Wasafi Classic Baby (Wcb), Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ Ametajwa Mara Nyingi Zaidi Kwamba, Anataka Kujitoa Kwenye Lebo Hiyo.

 

Haya Ni Madai Ya Muda Mrefu. Yanaungwa Mkono Na Viashiria Mbalimbali Ambavyo Watu Wamekuwa Wakiunga Doti.

Kama Ni Kweli Madai Haya Yana Mashiko, Basi Rayvanny Anapaswa Kuchagua Kimoja. Mwanga Au Giza, Nyeupe Au Nyeusi.

 

Tetesi Za Rayvanny Kuondoka Wcb Iliyo Chini Ya Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Zilikuja Muda Mfupi Tu Baada Ya Staa Mwingine Aliyekuwa Chini Ya Lebo Hiyo, Rajab Abdul ‘Harmonize’ Kusema Mwishoni Mwa Mwaka Jana.

Harmonize Alivunja Mkataba Na Wcb Akiwa Ni Staa Wa Pili Baada Ya Richard Martin ‘Rich Mavoko’.

Madai Ya Rayvanny Kuondoka Wcb, Yamekuwa Yakitokana Na Kutoonekana Kwenye Matukio Muhimu Ya Memba Wengine Wa Lebo Hiyo.

 

Kinachoibua Sintofahamu Ni Kwamba, Katikati Ya Madai Hayo, Rayvanny Ameachia Mkwaju Mkali Wa Amaboko Akishirikiana Na Diamond, Lakini Hilo Halijafuta Tetesi Hizo. Badala Yake, Zinaendelea Kushika Kasi Kila Kukicha.

 

Hali Hii Inanifanya Kufikiri Kuwa, Huwenda Lisemwalo Lipo Na Kama Halipo, Basi Laja. Msemo Wa Kiswahili Unaofaa Hapa Ni ‘Ukiona Moshi Ujue Kuna Moto’!

Lakini Kama Kweli Rayvanny Amedhamiria Kusepa Wcb Na Kwenda Kuanzisha Lebo Yake Mwenyewe Kama Alivyowahi Kusema, Itakuwa Ni Namna Ya Kujipima Kile Alichokipata Kwa Diamond Kama Uzoefu Chini Ya Mabawa Ya Mwanamuziki Huyo Mkubwa Barani Afrika.

 

Kwa Hiyo, Kama Mawazo Ya Rayvanny Ni Hayo, Basi Itakuwa Ni Nafasi Yake Nyingine Ya Kuonesha Uwezo Wake Binafsi.

Hata Hivyo, Cha Muhimu Hapa Ni Kwa Rayvanny Kukumbuka Kwanza Na Kujiuliza, Je, Ana Uamuzi Mwingine Wa Kukaa Mezani Na Uongozi Wa Wcb Na Kusikilizwa Matakwa Yake? Kama Akisikilizwa Matakwa Yake Na Akapewa Anachokitaka, Je, Ana Sababu Nyingine Ya Kujitoa Wcb? Je, Sababu Hiyo Ni Nzito Kiasi Gani? Je, Ni Muda Sahihi?

 

Kwa Njia Hii, Rayvanny Anaweza Kumaliza Msigano Uliopo Kwenye Uamuzi Wake Wa Kuondoka Wcb Ambapo Ni Pata-Potea, Kwani Hakuna Uhakika Wa Huko Aendako Ukizingatia Atakuwa Ameondoka Kwenye Lebo Kubwa Ya Muziki Inayotolewa Macho Na Wanamuziki Wengi Nje Na Ndani Ya Tanzania. Kuna Wasanii Wengi Wa Nchini Kenya Wamekuwa Wakitamka Waziwazi Kwamba, Wanatamani Wcb Iwe Na Tawi Nchini Humo Ili Wajiunge Nayo.

 

Rayvanny, Kama Anataka Kwenda Kujikita Kwenye Lebo Yake Ya Surprise Music, Anapaswa Kujua Kwamba, Sasa Atakuwa Hawazi Kuimba Tu, Bali Itamlazimu Kufanya Mambo Mengine Ya Utawala.

 

Kama Ndicho Anachokitafuta Rayvanny, Anapaswa Kuwa Na Uhakika Kwamba, Endapo Atavunja Mkataba Na Wcb Haendi Kuuweka Muziki Wake Rehani.

Kwenye Uamuzi Kama Huu, Rayvanny Anapaswa Kujifunza Na Kuwa Makini Mno Kutoka Kwa Harmonize Ambaye Naweza Kusema Amefanikiwa Kwa Kiasi Fulani, Ambapo Baada Ya Kuondoka Wcb, Alikwenda Kuimarisha Lebo Yake Ya Konde Gang Music Worldwide.

 

Kama Rayvanny Hajui, Harmonize Alipoamua Kujitoa Wasafi, Alifanya Hivyo Baada Ya Kujiaminisha Huko Aendako Ni Salama Kwa Ajili Ya Afya Ya Muziki Wake.

 

Matokeo Yake, Pamoja Na Jitihada Zote, Lakini Bado Harmonize Hajafikia Levo Ya Diamond Pamoja Na Kwamba Amekubalika Kwa Rais Wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli.

 

Katika Mazingira Kama Haya, Rayvanny Anapaswa Kujipa Muda Wa Kuutafakari Kwa Kina Uamuzi Wake Huo Wa Kujitoa Wcb Ikiwemo Kutafuta Watu Sahihi Wa Kuwekeza Kwenye Muziki Wake Kama Ilivyo Kwa Harmonize.

 

Umakini Wa Rayvanny Ni Muhimu, Kwani Anaweza Kuchanga Karata Zake Vizuri Akawa Kama Harmonize, Lakini Akikosea Aina Ya Karata Ya Kulamba, Basi Anaweza Kujikuta Amepita Kwenye Mazingira Kama Ya Rich Mavoko Ambaye Hadi Sasa Anahangaika Kurudi Kileleni.

 

Wadau Wa Burudani, Wanafahamu Ni Nini Kilimpata Rich Mavoko Baada Ya Kuvunja Mkataba Na Wcb. Hadi Leo Kila Mdau Anaumia Juu Ya Kupotea Kwa Kipaji Kikubwa Cha Rich Mavoko –Messi Wa Bongo Fleva!

Dondoo;

Jina Kamili: Raymond Shaban Mwakyusa

A.K.A: Rayvanny/Vanny Boy

Tarehe Ya Kuzaliwa: Agosti 22, 1993

Mahali Alipozaliwa: Mbeya

Umri: Miaka 27

Kazi: Muziki

Ndoa: Hajaoa

Mtoto: 1

Makala: Sifael Paul

Leave A Reply