The House of Favourite Newspapers

Kama Una Kipaji Cha Soka, Nenda Stand United

0

 

KOCHA wa Stand United, Athuman Bilali ‘Billo’ amewaita vijana wenye vipaji vya kucheza soka kwa ajili ya kufanya majaribio na watakaofanya vizuri basi watasajiliwa kwenye kikosi hicho tayari kwa kuwatumia msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

 

Bilo aliliambia Championi Ijumaa kuwa, tayari programu ya majaribio kwa wachezaji imeshaanza hivyo ni vyema vijana wenye vipaji wakaendelea kujitokeza kuonesha vipaji vyao ili waweze kupata nafasi ya kusajili katika timu hiyo.

 

Bilo alisema licha ya timu hiyo kuwa katika hali ngumu kiuchumi, anaamini watafanya usajili mzuri kwani kuna vijana wengi wenye vipaji lakini hawapati nafasi ya kucheza kitu ambacho kinawafanya waamini watafanya usajili mzuri ambao utaleta ushindani wa hali ya juu kwa timu zitakazoshiriki ligi kuu msimu ujao.

 

“Tayari tumeshaanza kufanya majaribio ya wachezaji kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu hivyo tunatoa wito kwa vijana wenye vipaji kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini wajitokeze kwa wingi ili waweze kuonesha vipaji vyao na wale watakaofanya vizuri tutawasajili katika kikosi chetu cha Stand United,” alisema Billo.

 

IDD MUMBA | CHAMPIONI | MWANZA

Leave A Reply