The House of Favourite Newspapers

KAMA UNASUMBULIWA NA GESI TUMBONI TUMIA ALOE VERA

LEO kwenye safu yetu ya tiba kwa chakula tutaona jinsi ya kutibu gesi nyingi tumboni tatizo ambalo uwakumba wengi, wapo wanaodhani kuwa na gesi tumboni ni sababu ya vidonda vya tumbo si kweli, wakati mwingine gesi huuma na kukufanya wewe uhisi hivyo.  

 

Cha muhimu ni kumcheki daktari ili achukue maelezo yako na kukupima ukweli utatoka kwenye vipimo, hapa leo nimekuletea tiba ya gesi iwapo ikikutokea una gesi utatumia kama zifuatavyo.

Aloe vera ni mmea ambao ni rahisi kuupata unatibu magonjwa mengi lakini na hili la gesi tumboni ni moja ya magonjwa yanayotibiwa. Unachotakuwa kufanya ni kuichuna upate ute wake kwenye kijiko cha chakula, changanya na juisi au maji ya nazi kisha kunywa dakika 15 mpaka 20 kabla ya kula chakula. Fanya hivyo kila siku mpaka utakapopona ugonjwa huo wa gesi umeisha.

Ndizi mbivu na Papai

Matunda haya ni mazuri yatakupa nafuu iwapo utakuwa unasumbuliwa na ugonjwa wa gesi kwani yatakusaidia kufanya mmeng’enyo wa chakula kiurahisi, watu wengi wenye gesi tumboni hupatwa na tatizo la ukosefu wa choo hivyo ukuwa na uwezo wa kuyapata matunda haya yatakusaidia.

Tangawizi

Tangawizi inatibu kizunguzungu lakini hata tatizo hili la gesi inao uwezo wa kukutibu kwani inasaidia kusagwa kwa chakula tumboni. Kama unahisi unagesi nyingi tumboni kunywa chai yenye tangawizi itakusaidia kuondoa tatizo hilo.

Comments are closed.