Kamanda Mambosasa Awavalisha Vyeo Askari Saba – Video

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa amewavalisha vyeo askari saba wa jeshi hilo waliyopandishwa vyeo na IGP Simon Sirro, Desemba 2018, kutokana na utendaji kazi mzuri katika majukumu yao.

 

Zoezi hili limefanywa leo Jumatano, Januari 9, 2019 na Kamanda Lazaro Mambosasa, kwa niaba ya IGP Sirro katika uwanja wa kituo cha polisi Osterbay, kwa kuwavalisha rasmi vyeo hivyo ya nafasi ya koplo.

Askari hao ni;

  1. F8889 DETECTIVE CONSTABLE PHILIP
  2. G5128 DETECTIVE CONSTABLE HASSAN
  3. G6712 DETECTIVE CONSTABLE DOMINIC
  4. WP8038 DETECTIVE CONSTABLE HAPPINESS
  5. H604 DETECTIVE CONSTABLE SAMWEL
  6. H3286 DETECTIVE CONSTABLE NICKO
  7. WP11541 DETECTIVE CONSTABLE IRENE.

Mambosasa alianza kwa kukagua Gwaride Imara la Jeshi la Polisi kikosi cha kutuliza ghasia Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

 

Aidha, Mambosasa amewapongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na viongozi mbalimbali wa jeshi hilo kwa kufanya kazi nzuri na kwa ushirikiano mwaka 2018 hali iliozidi kuimarisha ulinzi na usalama wa Jiji la Dar es Salaam.

 

Hata hivyo, Mambosasa ametoa rai kwa polisi na wananchi wa Mkoa wa Dar kuongeza mshikamano ndani ya mwaka 2019 ili kuimarisha usalama zaidi wa mkoa huo huku akitoa shukrani za dhati kwa baadhi ya Makampuni binasfi ya ulinzi yanayoshirikiana na polisi katika kuimarisha ulinzi.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

KARIBU ujiunge na familia ya marafiki wa Global TV Online – Club sasa, uwe wa kwanza kupata video zote za Global TV, video za hamasa kutoka kwa Eric Shigongo, breaking news za matukio yote duniani, michezo na dondoo za afya. Utapata nafasi ya kuingia bure na kutazama shoo, matamasha, semina na burudani zinazoandaliwa na Global TV mikoa yote Tanzania.
Pia, ukiwa na tatizo la kifamilia mfano misiba, kuuguliwa na majanga, marafiki zako wa Global TV Club tutakusaidia.
 
Pia, tutakuunganisha na mtandao wa marafiki zetu waliyofanikiwa ndani na nje ya Tanzania, ili upate mafunzo maalum ya kujikwamua kutoka katika hali duni ya maisha.

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

VIDEO: SHUHUDIA TUKIO HILO

Loading...

Toa comment