The House of Favourite Newspapers

Kamanda wa polisi Mkoa wa Lindi Azungumzia Ajali ya Basi la King Yasini na Lori La Mizigo

Kamanda wa polisi Mkoa wa Lindi kamishna msaidizi wa jeshi la polisi (ACP )John Imori amethibitisha kutokea kwa ajali ya gari la Abiria na mizigo iliyotokea Leo tarehe 06/11/2024 saa 5:10 asubuhi katika Kijiji Cha Ruhokwe kata ya Mnolela Mkoani Lindi.

ACP John Imori magari mawili yaliyo sababisha ajali hiyo ni Basi lenye usajili No T557 EAG aina ya Stangrong la kampuni ya King Yasini ambayo ilikua ikifanya safari za kutoka Mtwara kuelekea Dar es salaam,kugongana na Lori lenye usajili No T631 AER aina ya Scania ambalo likifanya safari zake kutokea masasi kuelekea Mtwara.

Aidha ACP John Imori Amesema gari la abiria lilikua na jumla ya abiria 53 na wafanyakazi wawili ambao ni kondakta na wakala na kwa upande wa Lori pia lilikua na abiria wawili ambao ni Tingo na mwingine mmoja ambae alikua alikua anasindikiza mzigo kutoka masasi kuelekea Mtwara.

Kamanda wa polisi amesema Kutokana na ajali hiyo imesababisha majeruhi watatu wawili ambao ni kondakta na wakala ambao wametokea kwenye basi na kwenye Lori ni Tingo pekee na kufanya jumla ya majeruhi watatu ambao tari wamepelekwa hospitali ya Nyangao kwa matibabu.

“Chanzo Cha ajali ni uzembe wa dereva wa King Yasini kujaribu kulipita Lori lingine bila kuchukua tahadhari”Amesema ACP John Imori

Nae Athumani Mohamed Dereva wa Lori mkazi wa Nachingwea Mkoani Lindi Amesema chanzo Cha ajali ni dereva wa basi kutaka kulipita lori na kusababisha ajali hiyo.

“Basi lilikua limeongozana na Lori na Mimi na Mimi nilitaka kupishana na Lori ambalo lilikua limeongozana na basi kwahiyo katika kupishana Lori huyu wa basi ndiyo alikua ana over take Lori tayari tayari tukawa tumegongana.”Amesema Dereva wa Lori

Nae shuhuda wa ajali Nolascus Mrope Shuhuda wa ajali mkazi wa Mtwara ambae alikua abiria wa basi amesema dereva wakati anataka kulipita Lori ambalo lilikua limewatangulia ndipo lilitokea lori lingine mbele ambalo dereva wa basi hakuliona na kusababisha ajali hiyo.