Kamati Kuu ya CCM Yapitsha Majina ya Wagombea Nafasi Mbalimbali

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imekutana Machi 10, 2025, Jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine imepitisha majina ya Wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi zilizokuwa wazi ndani ya CCM na Jumuiya zake kwa nafasi za Wilaya na Mikoa.