The House of Favourite Newspapers

KAMATI MASTAA BONGO YAPASUKA

DAR ES SALAAM: Wakati staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa kwenye maandalizi ya kuwaandalia usafiri wa ndege ya kuwabeba mastaa wa Bongo waliokuwa wameunda kamati ya sherehe ya mtoto wa mtangazaji Zamaradi Mketema kwa ajili ya kwenda kusherehekea siku hiyo ya kuzaliwa kwa binti yake Latiffa ‘Tiffah’ kama alivyowaahidi, kamati hiyo imeonekana kupasuka kwani wapo wanaosema watakwenda lakini wengine wamekataa.

TUJIUNGE NA CHANZO

Kwa mujibu wa chanzo kilicho ndani ya kamati hiyo (jina linahifadhiwa), mbali na kugawanyika huko, wapo wanakamati waliomgwaya Zari kutokana na maneno aliyowatolea mtandaoni kwamba wabaki wasiende Sauz kumchafulia nyumba.

“Kamati ya maandalizi ya sherehe ya mtoto wa Zamaradi ambayo ilipewa mualiko wa kwenda kusherehekea sherehe ya binti wa Zari imeonekana kupasuka kwani wapo wanaosema hawaendi lakini wapo wanaosema watakwenda kama kawaida wanasubiri tu mipango ikamilike.

“Kule kumewaka moto wapo wanaotamani kwenda kwa sababu wengine hawajawahi kufika Sauz baada ya kutangaziwa vile walifurahi, lakini baada ya mzazi mwenzake Diamond, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kuwaambia watakwenda kuchafua wengi wao wamegwaya kwani wanaogopa kufukuziwa mlangoni,” kilisema chanzo hicho.

AMANI LAWASAKA

Hata hivyo, Amani lilikwenda mbele zaidi na kuamua kuwasaka baadhi ya mastaa waliokuwemo kwenye kamati hiyo ambapo kila mmoja aliongea la kwake kama ifuatavyo;

FAIZA: NILIJUA SITAKWENDA

Msanii wa filamu na mjasiriamali, Faiza Ally alisema kuwa alijua wazi kuwa hatakwenda kwa sababu Zari ‘alishamblock’ siku nyingi kwenye ukurasa wake wa Instagram. “Mimi baada ya kutangaziwa vile tu nilijua siwezi kwenda kwa sababu Zari alishaniblock siku nyingi, sasa huwezi kwenda kwa mtu ambaye alishakublock na alivyosema maneno yale ndio kabisaaa,” alisema.

MAIMARTHA: TABIA YA ZARI SIKUIPENDA

Mtangazaji Maimartha Jesse yeye alipoulizwa amejipangaje alidai kuwa hawezi kwenda kwa sababu hakuipenda tabia ya Zari kuwaambia kuwa watakwenda kumchafulia nyumba.

“Sikuipenda kabisa tabia ya Zari, yeye angeacha akaona kama kweli tutaenda au la lakini kabla hata siku hajizafika akajibu palepale, ya nini kwenda? Nimemshangaa maana hajui kama kwake tungeenda ingekuwa na faida sana hata kujitangaza kibiashara.”

ESTER KIAMA: NINGEENDA NINGEVAA SOKSI

Staa wa filamu za Kibongo Ester Kiama alidai kuwa hakufurahishwa na vijembe vya Zari lakini hata angeenda angevaa soksi ili asichafue nyumba.“Sitarajii kwenda ila hata kama ningekwenda ningevaa soksi nyumbani kwake maana sikuelewa kwa nini amesema tutamchafulia nyumba,” alisema Ester.

SHAMSA: ILE ILIKUWA NI KIKI TU.

Shamsa Ford yeye alidai kuwa anachojua lile tangazo la wao kwenda Sauz kwenye sherehe ya Tiffah ilikuwa ni kiki tu wala hakukuwa na ukweli wowote. “Unadhani mchezo kuwasafirisha watu wote wale, ile ilikuwa ni sehemu ya kiki tu, wala siendi mimi,” alisema.

WOLPER: SINA TATIZO NA NA ZARI

Mbunifu wa mavazi na muigizaji, Jacqueline Wolper yeye alidai kuwa hana tatizo na Zari kabisa, wanaheshimiana iwapo atakuwa amerejea kutoka shule ambapo anasoma kwa sasa, atakwenda tu. “Shule ndio inaweza kunizuia lakini nikiwa nimerejea nitakwenda tu kwani sina tatizo na Zari,” alisema Wolper bila kuanisha shule anayosoma na kitu anachosomea.

WENGINE KUIBUKA

Hata hivyo, Amani lilipowatafuta Zamaradi na Aunt Ezekiel bila mafanikio, lilimpata mtu wa karibu na wawili hao ambaye alidai kuwa anachojua wanakamati hao pamoja wenzao wachache watakwenda kutokana na sababu zao binafsi.

“Si mnajua kuwa Zamaradi kwa sasa anafanya kazi na Wasafi TV na ndio mkurugenzi wa vipindi hawezi kukosa, na Aunt atakwenda kwa sababu ya mzazi mwenzake Mose Iyobo ile ni familia ya Wasafi. “Kama hiyo haitoshi, kuna wengine hawataki kujulikana wapo upande gani lakini siku hiyo wataenda, wanaogopa kuonekana wasaliti kwa wenzao,” alisema mtu huyo.

WEMA: MSIFIKIRI NAKWENDA

Aidha, Wema naye akiwa kama mwenyekiti wa kamati hiyo alidai kuwa hafikirii kwenda huko, alikuwa akichangamsha tu baraza. “Mimi sitarajii kwenda huko kabisa nimeshamuwishi Tiffah inatosha mimi huwa sina hiyana,” alisema Wema.

TUJIKUMBUSHE KIDOGO

Bethidei ya Tiffah ya kutimiza miaka 3 ilikuwa juzi (Jumatatu) lakini baba yake anatarajia kumfayia pati kubwa Agosti 17, mwaka huu ambapo alitangaza sherehe hiyo kuhudhuriwa na watu kibao wakiwemo mastaa wa nje pamoja na kamati hiyo ya mastaa kutoka bongo

Stori: Mwandishi Wetu, Aman

Comments are closed.