The House of Favourite Newspapers

Kambi ya Yanga Kigamboni Kiboko; Tazama ‘Mapicha’!

0

TIMU ya Yanga imehamishia kambi yake eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye majengo maarufu ya Avic yaliyojitenga na yenye utulivu mkubwa na vifaa kibao vya michezo, ukiwemo uwanja wa ndani kwa ndani na hakuna mgeni anayeruhusiwa kuingia ndani bila ruhusa maalumu.

Imehamishwa kutoka  Hoteli ya Regency Park, iliyoko Mikocheni,  na bilionea wa GSM, Ghalib Mohamed,  ili wapate maandalizi yenye utulivu tayari kwa kuanza msimu mpya.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya Yanga, tajiri huyo ameamua itakuwa inaishi hapo kuanzia sasa na hakuna habari ya hotelini tena kwani hapo ni pazuri zaidi na kocha amepakubali.

Ukifika eneo hilo unakutana na ukuta mrefu na ndani yake tena kuna ukuta mwingine uliopishana kama nusu kilomita na ndani ya ukuta wa pili ndimo kuna majengo mbalimbali ya makazi mapya ya Yanga.

Kocha wa Yanga, Zlatko Krmpotic, amesema timu hiyo inahitaji angalau mwezi mmoja ili icheze kwa kiwango anachotaka huku akiwasifu wachezaji wake kwa kuonyesha kiwango bora katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir ya Burundi.

Zlatco alisema wachezaji wake katika kilele cha Wiki ya Mwananchi, walijitahidi ingawa bado hapakuwa na muunganiko na wataitumia wiki moja iliyobaki kurekebisha mapungufu kabla ya kuanza kwa Ligi Septemba 6.

“Ninachowaahidi hapa kwangu ni kazi na nidhamu, huo ndiyo mwongozo wangu,” alisema Zlatko na kuongeza kwamba Yanga inahitaji mazoezi zaidi ili kutengeneza muunganiko mzuri na icheze kwa ubora mkubwa.

“Si kazi rahisi kupata muunganiko wa timu kwa muda mfupi hivi, ukizingatia timu ina wachezaji 14 wapya, hivyo inahitaji muda ili kuzoeana.

“Licha ya kwamba muda ni mfupi, tutatumia wiki moja iliyobaki kuyafanyia kazi mapungufu yetu ili tuanze vizuri ligi, lakini ili timu icheze kwa ubora wake inaweza kuchukua mwezi mzima ili kuwafanya wachezaji wote kuzoeana na kucheza kwa maelewano,” alisema Zlatko.

“Nimewaangalia wachezaji wote waliosajiliwa wana vipaji vikubwa,  muhimu wanatakiwa kujitoa kwa ajili ya timu na kuwa na nidhamu ndani na nje ya uwanja,” alisema Zlatko.

 

Leave A Reply