The House of Favourite Newspapers

Kamera Kuwanasa Watumia Simu Barabarani

0

AUSTRALIA imekuwa nchi ya kwanza kuzindua mfumo wa kamera za barabarani (za roboti) ili kuwanasa madereva wanaotumia simu wakati wakiwa wanaendesha magari.

 

Kamera hiyo iliyotengenezwa kwa roboti (Artificial Intelligence AI) itawapiga picha madereva wanaotumia simu au kufanya mambo mengine yasiyoeleweka.

Mfumo huo umeanza kufungwa katika jimbo la New South Wales, ili kuwasaidia askari wa usalama barabarani kukabiliana na madereva wanaovunja sheria.

 

Msemaji wa Wizara ya Usafirishaji amesema kamera hizo zitafanya kazi usiku na mchana na hazitaathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Dereva atakayetiwa hatiani atatozwa faini ya TZS 541,100, na kuwekewa alama tano za hati chafu kwenye leseni.

Leave A Reply