The House of Favourite Newspapers

Kampeni S/Mitaa Makalla Aacha Ujumbe Mzito Kigamboni

0

“Niwapongeze wanachama wa CCM wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha, Mkoa huu ni miongoni mwa mikoa kumi iliyoongoza kujiandikisha, niwapongeze na niwatake siku ya kupiga kura tarehe 27, 11, 2024 muoneshe Demokrasia ya kweli kwa kupiga kura.

“CCM imewaletea wagombea safi, watakaowaletea maendeleo,  nawaomba mkipigie chama cha Mapinduzi kwa maendeleo ya taifa.

Kama Chama Kiongozi, Chama Kilichopo madarakani, hakuna nafasi ya kuwaachia wapinzani, tumeweka wagombea kila mtaa nchi nzima, tuwahakikishie watanzania kuwa tumejipanga kuwaletea maendeleo.

“Uchaguzi huu ni muhimu sana, uchaguzi huu ni muhimu sana pale Dkt. Samia Suluhu Hassan anapoleta pesa ya maendeleo na kuelekeza kwenye miradi ambapo husimamiwa na mwenyekiti kwani ndiye atakayeongoza katika kuonesha sehemu ya ujenzi wa mradi husika”.

“Wagombea hawa ni muhimu sana kwa sababu maendeleo yanayoletwa ni chimbuko la yeye na wananchi kwa kuunganisha nguvu za pamoja”

Leave A Reply