The House of Favourite Newspapers

Kampeni Ya Vimba na Timiza Akiba Droo Ya Pili Washindi 50 Wapatikana, Wiki Ijayo Flat Sceen

0
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (katikati) akizungumza muda mfupi kabla ya kuchezeshwa droo hiyo. Kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha na kulia ni Msimamizi wa Masoko, Mawasiliano na Huduma kwa Wateja kutoka Benki ya Letshego, Selestino Nachenga.

Dar es Salaam, 20 Aprili 2023: Kampeni ya Vimba na Timiza Akiba inayoendeshwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na Benki ya Let shego leo imeendelea kwa kuchezesha droo ya pili ambapo washindi 50 wa pesa taslimu shilingi elfu ishirini wamepatikana.

Akizungumza baada ya kuwapata washindi hao Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema wanafuraha kubwa kuchezesha droo hiyo na kuwazawadia zawadi zao wateja wao.

Mmbando alisema jinsi ya kushiriki bahati nasibu hiyo jambo la kwanza uwe mtumiaji wa mtandao wa Airtel na uwe unaweka akiba kupitia huduma ya Timiza Akiba. Aliendelea kusema;

Meneja wa Huduma za Airtel Money Hellen Lyimo (katikati) akimpigia simu mmoja wa washindi kumpa habari ya ushindi wake.

“Ili uweke pesa kwenye Timiza Akiba na kuingia kwenye droo na uweze kujishindia zawadi mbalimbali unachotakiwa ni kupiga *150*60# kisha unachagua namba 6 halafu unachagua namba 1 kisha namba 3 unaweka akiba yako hivyo nawe unakuwa umeingia kwenye droo ya kuweza kujishindia zawadi mbalimbali.

“Promosheni hii inadumu kwa wiki nane na wiki zote hizo tunakuwa tukitoa zawadi, leo tunatoa zawadi kwa washindi 50, wiki ijayo tunatoa zawadi kwa washindi 25 ikiwemo Tv ya kisasa flat creen.

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akiangalia namba ya mshindi iliyojitokeza kwenye screen baada ya kuibuka na ushindi, kulia ni Selestino Nachenga wa Benki ya Letshego.

“Wiki nyingine ijayo tunatoa mshindi wa pikipiki na wiki ya mwisho tunafunga shindano letu kwa kutoa zawadi ya Bajaj mpya kabisa”. Alimaliza kusema Mmbando na kuwataka watumiaji wa simu za mkononi kutumia mtandao wa Airtel ili waweze kujiwekea akiba.

Leave A Reply