The House of Favourite Newspapers

Kampeni zamkosesha mtoto Baba Haji

0

BABAHAJINAWEMA1.jpgMayasa Mariwata

MSANII wa filamu Bongo, Haji Adamu ‘Baba Haji’ amesema kampeni za siasa zilizokuwa zikifanyika kuelekea uchaguzi mkuu uliopita, zimemkosesha kupata mtoto kwa vile alikuwa mbali na mkewe aliyebaki Dar.

Akizungumza na gazeti hili, alisema alipata mtoto mmoja wa kiume katika uhusiano wake kabla hajamuoa mwanamke huyo, lakini akakosa amani kwa sababu ya hamu yake ya kupata mtoto wa kike.

“Natamani hata kesho mke wangu anizalie mtoto wa kike yaani namsaka kwa udi na uvumba, huenda ningekuwa nimeshampata lakini mambo ya uchaguzi yalisababisha zoezi langu lisiende na wakati, sababu muda mwingi nilikuwa bize kwenye mambo ya kampeni huku bibie akibaki Dar wakati mimi nikizunguka mikoani, hivyo sasa hivi nafanya jitihada za hali ya juu,” alisema.

Leave A Reply