The House of Favourite Newspapers

Kampuni inayongeneza dawa za Ukimwi yapandishwa bei kwa asilimia 5000

0

DaraprimqTembe za Daraprim.1217_martin-shkreli-finance_416x416
Mkurugenzi mkuu waKampuni ya Turing Pharmaceuticals Martin Shkreli

Kampuni ya Turing Pharmaceuticals inayotengeneza madawa muhimu duniani, imepandisha gharama ya dawa inayotumika kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi kutoka dola za Kimarekani 13.50 hadi dola 750 sawa na Tsh. 28400 hadi Tsh. 1,575,000 ambazo ni ongezeko la asilimia 5000.

Turing Pharmaceuticals imelaumiwa na wadau wa maswala ya Ukimwi kwa kuongeza bei ya dawa hiyo ya Daraprim ambayo imekuwa mstari wa mbele katika kuimarisha uwezo wa mwili wa mgonjwa aliyeathirika kupigana na maambukizi mapya.

Turing Pharmaceuticals ilinunua hati miliki ya dawa hiyo ya Daraprim mwezi uliopita Agosti.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Martin Shkreli amenukuliwa akisema kuwa faida itakayopatikana baada ya mauzo ya dawa hiyo itasaidia kugharamia utafiti wa dawa mpya na zenye ubora zaidi.

Tembe moja ya dawa hiyo ya Daraprim inagharimu dola moja pekee kutengeneza.

Hata hivyo bwana Martin Shkreli anasema kuwa bei hiyo haijumuishi gharama ya kunadi dawa hiyo wala usambazaji wake ilihali gharama imeimarika maradufu katika miaka ya hivi punde.

”Katika siku za hivi punde dawa za kupunguza makali ya saratani zinagharimu dola laki moja (100,000) ilhali gharama yake asili inaweza kugharimu dola nusu milioni.

Daraprim inauzwa kwa bei nafuu zaidi ikilinganishwa na dawa zinazotibu magonjwa sawa.

Shkreli aliiambia runinga ya Bloomberg katika mahojiano ya kibinafsi.

Shkreli alimsuta mwandishi mmoja wa habari kupitia mtandao wa Kijamii akimuita kuwa ”mjinga” kwa kutaka kujua kwanini kampuni yake ilikuwa inaongeza maradufu bei ya dawa hiyo muhimu katika vita dhidi ya Ukimwi haswa katika mataifa maskini duniani.

Daktari Wendy Armstrong kutoka muungano wa wauguzi nchini Marekani HIV Medicine Association amekashifu sababu zilizotolewa kwa ajili ya nyongeza hiyo kubwa ya bei ya dawa hiyo.

Bi Hillary Clinton anayewania cha urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic ameonya kuwa, endapo ataingia madarakani, serikali yake itachukua hatua kali dhidi ya makampuni yanayofaidi kutokana na msiba wa watu kwa kupandisha bei ya madawa maalum.

JIUNGE NA GLOBAL BRAKING NEWS UPATE HABARI KEMKEM ZA UCHAGUZI MKUU

globalbreakingnews.JPG

Leave A Reply