Kampuni ya Kilombero Yaibuka Kidedea Tuzo za ATE 2022
DAR ES SALAAM, Kampuni ya Sukari ya Kilombero imefanikiwa kunyakua tuzo katika kipengele cha Uanagenzi na Mafunzo (Apprenticeship and Internship) huku ikishika nafasi ya pili katika kipengele cha Ushirikishwaji wa Watanzania (Local Content) na kupokea cheti cha shukrani kwa kudhamini hafla hiyo wakati wa tuzo zitolewazo na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) zilizofanyika Disemba 2, 2022 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam