Kampuni ya Meridianbet Waunga Mkono Kampeni ya Buku ya Hedhi Salama
Meridianbet wameunga mkono jitihada za kampeni ya Buku ya Hedhi salama inayoratibiwa na Shufaa Hemed Nasoro.
Kampeni hii ilikuwa imelenga kuchangisha michango ya kiwango cha angalau shilingi elfu moja kuwasaidia mabinti ambao wanapata changamoto za kumudu gharama za taulo za kike.
Meridianbet, ambao ni wadau wakubwa wa shughuli za kijamii, wanaona umuhimu wa hedhi salama kwa mabinti, na katika kuhakikisha hilo linafanikiwa hawakusita kuwashika mkono waratibu wa kampeni hii.
Kampeni hii inawalenga mabinti na wanawake wanaoshindwa kumudu gharama za taulo za kike Tanzania nzima, waratibu wakiwa wanalenga kuyafikia maeneo mengi yenye uhitaji ikiwa ni pamoja na vijijini.
Wakati kampeni ikitoa fursa ya kila mtu kuchangia kwa kutoa mchango wa shilingi elfu moja kuiwezesha kampeni hii, Meridianbet wametoa boksi 16, na kila boksi ikiwa na pakiti 30 za taulo za kike.
Akizungumza kwa niaba ya Meridianbet, Meneja wa Masoko wa Meridianbet bwana Twaha Mohammed amesema wanafurahi kuwaongezea kujiamini.
“Sisi tumekuwa na kawaida ya kuwashika mkono ndugu zetu wanaokuwa na mahitaji. Tunayatazama makundi maalumu na kuwapa thamani. Tunaamini kwa kwa hili la taulo za kike, walengwa watapata kuwa salama na kurejesha kujiamini.”
Kwa upande wa Mratibu wa kampeni hii ya Buku ya Hedhi Salama, Shufaa Hemed Nasoro amesema kuwa anaishukuru Kampuni ya Meridianbet kuwa mmoja wa wadau wanaokuwa mstari wa mbele kuwasaidia mabinti.
“Nimefurahi sana, nawashukuru Meridianbet kwa mchongo wao. Hili ni jambo jema kwa kuwa tunaenda kuwasaidia mabinti na wanawake ambao wana uhitaji, ili wawe salama wakati wa hedhi, lakini pia kuwapa uwezo wa kujiamini kufanya shughuli zao bila wasi wasi”
Meridianbet ni Kampuni kongwe ya ubashiri wa mtandaoni Tanzania, wakiwa wanatoa huduma za ubashiri wa mtandaoni wa michezo ya kawaida na Kasino ya Mtandaoni.