Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya BETWINNER Yazinduliwa Rasmi Tanzania
Kampuni ya michezo ya kubashiri ya Betwinner imezinduliwa rasmi nchini Tanzania, ikileta fursa mpya na za kipekee kwa wateja wa michezo ya kubahatisha.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi Mkuu wa Betwinner, Jesse Ndambala, alisema kuwa ujio wao umelenga kuwapa wateja Odds nzuri zaidi kulinganisha na kampuni nyingine za kubashiri.
Ndambala alisisitiza kuwa Bet Winner imeleta ubunifu mkubwa katika michezo yao ya kubashiri ikiwa pamoja na kuwapa asilimia 100 ya bonus kwa wateja wapya ikiwa ni sehemu ya ofa ya ukaribisho.
“Mbali na kuwa na odds nzuri, tumeweka ubunifu mkubwa katika michezo yetu, na kutoa asilimia 100 ya bonus kwa wateja wapya. Lengo hapa ni kuongeza burudani na chachu ya ushindani kwenye sekta ya michezo,” alisema Ndambala.
Alifafanua kuwa Betwinner imejipanga kukabiliana na ushindani katika sekta ya michezo ya kubashiri kwa kutoa huduma bora.
Kwa mujibu wa Ndambala, kampuni yao inatoa huduma za kisasa zinazomwezesha mshindi kupata fedha zake papo hapo baada ya mshindi kudhibitishwa.
“Tunaamini kuwa huduma zetu bora, zitawafanya wateja wetu kuichagua Betwinner kama kampuni pekee yenye kutoa huduma bora nchini Tanzania,” alisema.
Kampuni ya Betwinner ilianza biashara zake nchini Cyprus na inafanya kazi katika soko la kimataifa.
Kampuni hii pia imefanya kazi zake katika nchi kadhaa barani Afrika zikiwemo Kenya, Nigeria, Ghana, Zambia na Uganda.
“Kauli mbiu yetu ni ‘Ushindi kwa Washindi,’ na tumejipanga kuhakikisha wateja wetu wote wanapata ushindi kwenye kila michezo watakayoicheza na hivyo kuudhirisha kauli mbiu yetu,” alisema Ndambala.
Mbali na kutoa odds nzuri na bonus za ukaribisho, Betwinner pia imewekeza katika teknolojia za kisasa kuhakikisha kuwa taarifa na wateja zinalindwa kimalifu.
Kwa kuzingatia ushindani mkali katika sekta ya michezo ya kubashiri, Betwinner imeweka mikakati kabambe kuhakikisha kuwa wanakuwa mbele ya washindani wao.
“Tunayo timu ya wataalamu ambao wana uzoefu mkubwa katika sekta ya michezo ya kubashiri. Timu hii inahakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma bora na za kuridhisha,” alisema Ndambala.
Kampuni hiyo ilionyesha jinsi wateja wanavyoweza kubashiri michezo mbalimbali na kupata ushindi wa haraka na salama. “Tunataka wateja wetu wajue kuwa Betwinner ni chaguo sahihi kwao. Tunatoa huduma bora, za kisasa, na salama,” alieleza Ndambala.
“Tunaamini kuwa kwa kutoa huduma bora na za kisasa, tutaweza kuvutia wateja wengi na kuwa kiongozi katika sekta ya michezo ya kubashiri nchini Tanzania na kwingineko,” alimalizia Ndambala.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Michezo ya Bodi ya Kubahatisha nchini (GBT), James Mbalwe aliipongeza kampuni hiyo kwa kuongeza soko la ajira na vile vile kuchangia pato la taifa.
“Kuingia kwenu nchini kumesaidia kuongeza ajira, kwani naamini kuna Watanzania ambao wamepata ajira na vile vile kuongeza kipato kwa nchi na kuinua uchumi. Ila naomba kuwa waadilifu na kuwa na uwazi katika shughuli zenu. Mshindi akishinda, anatakiwa kupata zawadi yake, akikosa anajua kwa nini amekosa, hii itajenga uaminifu na kupata wateja wengi Zaidi pamoja na ushindani uliopo,” alisema Mbawe.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa shirikisho kampuni za michezo ya kubashiri Tanzania (TSBA) Sabrina Msuya aliipongeza kampuni hiyo kwa kuingia katika soko la Tanzania.
“Nawapongeza kwa kuingia katika soko la Tanzania na kuendeleza sekta hii ambayo kwa sasa inakuwa kwa kasi,” alisema Msuya.
Naye Mkurugenzi wa Masoko wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Aaron Nyanda aliipa angalizo kampuni hiyo kutotumia katika matangazo picha za wachezaji ambao hawana haki nazo ili kuepuka kuingia katika kesi ambazo zimetokea tayari na makampuni mengine kushindwa.
“Naomba, kama mna mpango kuwa na mabalozi, basi ingieni mikataba na wachezaji na kuwatumia katika matangazo yenu kwa mujibu wa sharia,” alisema Nyanda.