Kampuni ya Sukari ya Kilombero Yadhamini Tuzo za Consumer Choice Africa
KAMA mzalishaji mkubwa wa sukari nchini Tanzania, Kampuni ya Sukari ya Kilombero (KSCL) iliungana na watumiaji kutambua chapa na watu bora kwa kudhamini Tuzo za Consumer Choice Africa.
Baada ya mchakato wa kupiga kura, hafla ya kukabidhi tuzo hizo ilifanyika tarehe 12 Novemba katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.