The House of Favourite Newspapers

KAMPUNI ZA TANZANIA, KOREA ZASAINI USHIRIKIANO KATIKA UJENZI

Diwani Mathew Lubongeja (kushoto) akimkabidhi ramani na bendera ya Tanzania, Meya wa Jiji la Gyeongsan, ikiwa ni ishara ya ushirikiano wa miji ya Sengerema na Jiji la Gyeongsan katika masuala ya maendeleo.
Mkataba ukisainiwa na pande zote mbili.
Kiongozi wa kampuni ya Sungwoo I. D. Construction Co. Ltd ya Korea ya Kusini, Jeun Ki  Wook (kushoto) na Mkurugenzi wa kampuni ya JONTA Investment Ltd,  John Elias Ntalimbo (katikati) na Mathew Lubongeja wakionyesha hati za mkataba walioufikia.
Viongozi wa pande hizo mbili wakiwa katika mkutano.
Zoezi likiendelea.
Wakiwa katika picha ya pamoja.

 

KAMPUNI  mbili za Tanzania, Blue Mark iliyo chini ya Mkurugenzi wake, Eric Shigongo,  na JONTA Investment  Ltd  iliyo chini ya Mkurugenzi  John Elias Ntalimbo wa Shinyanga, zimesaini mkataba wa kuungana na kufanya kazi na kampuni ya Sungwoo I. D. Construction Co. Ltd ya  Korea ya Kusini inayoongozwa na Jeun Ki  Wook.

 

Mkataba huo umesainiwa jana Februari 27 jijini Daegu, Korea ya Kusini, baada ya mkutano wa siku mbili. Pia kumefikiwa makubaliano ya ushirikiano wa kimaendeleo baina ya mji wa Sengerema, mkoani Mwanza, na Jiji la Gyeongsan la Korea Kusini.

 

Zoezi hili limeratibiwa na diwani na mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri ya Wilaya  ya Sengerema, Mathew Lubongeja, ambaye kwa sasa yuko nchini Korea ambako imefahamika kwamba mkataba huo unahusu kukuza sekta ya ujenzi.

 

Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Rais wa Chuo Kikuu cha Yeungnam cha nchini humo, upande wa Tanzania ulitoa ombi la kukiunganisha chuo hicho katika ushirikiano na vyuo vikuu vya Sokoine na St.  Augustine ambapo ombi hilo lilikubaliwa.

 

Lengo la mkutano huo wa siku mbili lilikuwa ni kuwaunganisha wafanyabiashara wa Tanzania hususan wa tasnia ya ujenzi na makampuni ya Korea kushirikiana katika miradi mbalimbali.

 

Picha na: Esther Nakhayenze,  aliyepo Korea ya Kusini.

Comments are closed.