The House of Favourite Newspapers

Kamusoko atembeza mkwara mzito ligi kuu

0

kamusoko

Kiungo wa Yanga, Mzimbabwe, Thabani Kamusoko.

Hans Mloli,Dar es Salaam
KIUNGO wa Yanga, Mzimbabwe, Thabani Kamusoko, ameibuka na kutamba kuwa, bado ataendelea kuonyesha makali yake katika michezo inayofuata kwenye mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kamusoko ambaye aliitumikia Yanga katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara wikiendi iliyopita dhidi ya Coastal Union, amesema kwamba anauamini uwezo alionao na atazidi kujipanga kuhakikisha anafanya mazuri zaidi kila mechi iliyo mbele.

Kamusoko ameliambia Championi Jumatano kuwa, anafahamu kwamba ligi ni ngumu na ina changamoto kubwa lakini kwa mwanga aliouona katika mechi hiyo ya kwanza na morali aliyonayo, anaamini watafanya poa kwenye mechi zijazo.

“Huu ni mwanzo tu na kuhusu mechi iliyopita hiyo imeshapita, kinachoangaliwa sasa ni mechi zijazo ambazo nitahakikisha najituma nikisaidiana na wenzangu katika kuonyesha kiwango cha juu dhidi ya wapinzani wetu ili kuibuka na ushindi katika kila mchezo,” alisema Kamusoko aliyetua Yanga akitokea FC Platinum ya Zimbabwe.

Kiungo huyo, wikiendi iliyopita alionyesha kiwango cha hali ya juu sana wakati alipocheza kama kiungo mkabaji, wakati timu yake ikipopata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union.

Leave A Reply