Kamusoko na Ngoma Warejea Kuokoa Jahazi

Donald Ngoma.

MASTAA wa Yanga kutoka Zimbabwe, Thaban Kamusoko na Donald Ngoma wanaanza matizi rasmi na kikosi hicho leo Jumapili kujiandaa na mechi dhidi ya Mwadui FC, itakayopigwa Jumanne.

 

Wachezaji hao walikuwa wakifanya mazoezi maalum na sasa wanaanza mazoezi ya jumla na timu tayari kwa kucheza baada ya afya zao kuimarika. Walikaa nje ya uwanja kwa karibu miezi minne.

Thaban Kamusoko

Akizungumza na Spoti Xtra, Daktari wa Yanga, Edward Bavu alisema kuwa Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Amissi Tambwe ndio bado hali zao hazijatengamaa.

 

“Kamusoko na Ngoma wamemaliza programu maalum hivyo kwa sasa wanarejea rasmi mazoezi ya uwanjani na timu na uamuzi wa kutumika utabaki kwa benchi la ufundi kwamba wacheze au wasicheze. “ Ninja na Tambwe bado wanaendelea kupona,”alisema Bavu ambaye ni mzoefu kwenye tiba za wachezaji.

Loading...

Toa comment