The House of Favourite Newspapers
gunners X

Kanda Mikononi Mwa Mbelgiji Simba

0

MABOSI wa Simba wamefunguka kuwa, watamsikiliza kocha wao mkuu, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck juu ya nyota gani ambaye anamaliza mkataba wambakishe ikiwa ni baada ya kufanya tathmini yanguvu.

 

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa, ameweka wazi kwamba watalisikiliza benchi la ufundi juu ya nani ambao watabakishwa klabuni hapo kwa msimu ujao kutoka katika kundi ambalo linamaliza mikataba katika kikosi hicho.

 

Miongoni mwa nyota wa Simba ambao mikataba yao itamalizika mwishoni mwa msimu huu ni Deo Kanda, Hassan Dilunga, Yusuph Mlipili, Paul Bukaba, Mohammed Ibrahim na Shiza Kichuya.

 

Senzo ameliambia Spoti Xtra, kuwa watakaa na benchi la ufundi linaloongozwa na Sven kwa ajili ya kuwapa tathmini ya wachezaji gani ambao watatakiwa kubaki katika klabu hiyo kwenye kundi ambalo wanamaliza mikataba.

 

“Wale ambao watamaliza mikataba kabla ya kuwapa mipya ni lazima tumsikilize kocha na benchi lake la ufundi kuona ni nini ambacho wao wanakitaka.

 

“Huo ni mfumo ambao kila klabu ulimwenguni umekuwa ukiutumia ni lazima benchi la ufundi liseme ni kina nani ambao wanawataka kabla ya uongozi kufanya maamuzi,” alisema Mazingisa.

 

Leave A Reply