Kane Athibitisha Kubaki Spurs

NAHODHA wa Tottenham, Harry Kane amethibitisha na kusisitiza kuwa ataendelea kusalia ndani ya kikosi hicho.
Awali Kane
alikuwa anahusishwa na kujiunga na kikosi cha Manchester City ambao nao tayari walikuwa wamejipanga kumng’oa kikosini hapo.

 

Kabla ya kumalizika kwa Premier msimu wa 2020/21, Kane aliwahi kunukuliwa akisema sasa ni wakati muafaka kwa yeye kwenda kusaka makombe.

 

Nahodha huyo kwa sasa amesaliwa na miaka mitatu katika mkataba wake ndani ya Tottenham.

 

Kane alikuwa anataka kwenda Man City na alikosa mchezo wa kwanza wa Premier msimu huu akicheza ule wa pili dhidi ya Wolves ambao alipokelewa kwa shangwe na mashabiki wa timu hiyo.

 

Kane alisema: “Lilikuwa ni jambo kubwa kwangu kuona mashabiki wamenifurahia na kunipokea vizuri (Jumapili) na wakinipa ujumbe mzuri wa kuendelea kunisapoti. “Kwa hiyo nitaendelea kusalia ndani ya Tottenham msimu huu, kwa asilimia 100 nikiangalia zaidi namna ya kuisaidia timu yangu kufanya vizuri.”706
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment