The House of Favourite Newspapers

Kansiime Afunguka Kuachwa na Mumewe

Anne Kansiime na Mumewe Gerald Ojok

MVUNJA mbavu maarufu kutoka Uganda, Anne Kansiime ameamua kuvunja ukimya kwa kusema kuwa ameachwa na mumewe, Gerald Ojok.

Akifanyiwa mahojiano na katika kipindi cha TV nchini humo, Kansiime alitoa sababu za mumewe kumkimbia.“Nipo singo, naweza kuwa na mwingine, ratiba zangu zimebana sana, ieleweke nipo singo tu.

“Ni hivi, uhusiano wangu ulivunjika miezi sita iliyopita kabla dunia nzima haijajua, lakini naona presha inaniganda kwa muda mrefu. Nilikuwa naingiza kipato kikubwa zaidi yake, lakini sijui kama ni sababu ya yeye kunikimbia,” alisema Kansiime.

 

 

Comments are closed.