The House of Favourite Newspapers

Kante Nje Fainali ya FA

0

WAKATI Fainali ya Kombe la FA ikitarajiwa kupigwa leo kati ya Chelsea na Leicester City, kiungo wa Chelsea, N’Golo Kante atakosekana baada ya kupata majeruhi. Fainali ya FA itapigwa katika Dimba la Wembley leo Jumamosi saa 1:15 usiku ikiwa ni fainali ya pili mfululizo kwa Chelsea.

 

Kante atakosekana kwenye mchezo huo baada ya kuumia katika mchezo wa Premier dhidi ya Arsenal Jumatano iliyopita ambao walipoteza kwa bao 1-0. Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel ametihibitisha kukosekana kwa nyota wake huyo ambaye amekuwa chachu ya mafanikio ya kikosi hicho.

 

Tuchel alisema kiungo huyo hatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho (leo) kutokana na kuwa na majeruhi. “N’Golo ameachwa kwenye kikosi ambacho kitacheza fainali ya FA kutokana na kuwa na maumivu baada ya kuumia mchezo uliopita hivyo hawezi kucheza. “Huyo bado ana maumivu, lakini Mateo (Kovacic) pia hatakuwepo.

 

Kumchezesha Antonio Rudiger huenda tukamuweka kwenye hatari zaidi kutokana na haki yake kwa maana hiyo nitakosa mabeki wawili wa kati.” Tuchel leo ataiongoza Chelsea kwa mara ya kwanza kwenye Fainali ya Kombe la FA dhidi ya Leicester City.

Leave A Reply