Kanumba Feki Adaiwa Kuwa Mhamiaji Haramu

533615_398524800248797_1186715791_nMkali wa filamu Bongo, Rammy Gallis ‘Kanumba Feki’.

Mayasa Mariwata
Mkali wa filamu Bongo, Rammy Gallis ‘Kanumba Feki’ anadaiwa kuishi nchini bila vibali maalum, jambo linalomuweka hatarini muda wowote kuweza kutimuliwa Bongo kutokana na tumbuatumbua ya Serikali ya Rais John Pombe Magufuli inayoendelea.

Kwa mujibu wa chanzo, kuna hatihati kubwa ya msanii huyo ambaye wengi wamezoea kumuita Msomalia kufungashiwa virago kwani hana uhalali wa kuendelea kuwepo nchini.

“Yaani kwa hii kasi ya Mh. Magufuli sidhani kama Rammy atasalimika, si unaona jinsi ambavyo mzee wa kutumbua majipu yupo makini kwenye uongozi wake, yule kaka ni mkimbizi yaani akae tayari kwa safari ya kurudi kwao huko,” kilisema chanzo.

Baada ya kupata madai hayo, Showbiz Xtra ilimpo-vutia waya msanii huyo ili kusikia kauli yake kufuatia madai hayo alijibu;

“Mimi ni Mtanzania halali nina vigezo vya kuwepo Bongo, mama yangu ni Msomali baba ni Muarabu kachanganya na Mbrazil.”


Loading...

Toa comment