Kanye Akunja Mkwanja ‘Mkali Kuliko’ 2019

Related image

JARIDA la Forbes la Marekani limetoa orodha ya wanamuziki wa Hip Hop wanaolipwa mkwanja mrefu zaidi mwaka huu wa 2019, Kanye West akiingiza kwa mara ya kwanza mkwanja mrefu  ambao ni sawa na  Tsh. billioni 350 kuanzia mwezi Juni mwaka jana, 2018,  hadi Juni 2019.

Mkwanja huo mrefu umetokana na mauzo ya kampuni yake ya mavazi aina ya ‘YeezY’ ambayo yamekadiriwa kuingiza Dola bilioni 1.5.

Mwaka juzi nafasi hii ilikaliwa na rapa Jay-zZkwa wanamuziki akiwa ameingiza zaidi ya Tsh. billion 186.

Image result for kanye west yeezy company
Jarida la Forbes limeweka orodha ya marapa 20 bora walioingiza zaidi ya Tsh. trillioni 1.9 ambapo rapa wa mwisho ameingiza mkwanja Tsh. bilioni 41.  Orodha yenyewe hii hapa chini:

1. Kanye West ($150 million)
2. Jay-Z ($81 million)
3. Drake ($75 million)
4. Diddy ($70 million)
5. Travis Scott ($58 million)
6. Eminem ($50 million)
7. DJ Khaled ($40 million)
8. Kendrick Lamar ($38.5 million)
9. Migos ($36 million)
10. Childish Gambino ($35 million)
11. J. Cole ($31 million)
12. Nicki Minaj ($29 million)
13. Cardi B ($28 million)
14. Swizz Beatz ($23 million)
15. Meek Mill ($21 million)
16. Birdman ($20 million)
17. Future ($19.5 million)
18. Nas ($19 million)
19. Wiz Khalifa ($18.5 million)
20. Pitbull ($18 million).

Toa comment