The House of Favourite Newspapers

Kanye West Agawa Yeezy Boots kwa Mapaparazi

0

kanye-smileRAPA maarufu kutoka nchini Marekani, Kanye West ametimiza ahadi yake aliyoitoa Novemba mwaka jana ya kuwagawia viatu vya Adidas mtindo wa Yeezy (Yeezy Boosts) wapiga picha ‘mapaparazi’  ambavyo yeye ndiye mbunifu na wake.

Mwezi Novemba mwaka jana West aliwaambia, “Ipo siku nitawagawia ninyi nyote viatu vya Yeezy…. mwakani.”

jackMapaparazi hao wameonesha kufurahishwa na kitendo cha West kuwazawadia Yeezy Boosts huku wakimpongeza West na mkewe Kim Kardashian kwa moyo huo wa kuwasadia huku wengine wakisema imekuwa ni neema ya Krismasi.

Mpiga picha mmoja, Jack Arshakyan, aliyebhatika kupata zawadi hiyo aliandika hivi kwenye Instagram,”Shukrani nyingi ziende kwenu Kim Kardashian na Kanye West kwa kutuzawadia mimi na mapaparazi wenzangu Yeezy Boosts 350,” aliandika.

Leave A Reply