The House of Favourite Newspapers

Kanye West Aifuta Albamu Yake Mpya ya Swish

0

1405952708_kanye-west-zoom Kanye West

SWISH haipo tena. Ni baada ya rapa maarufu kutoka kiwanda cha muziki duniani, Kanye West kuamua kubadili jina la albamu yake mpya inayosubiliwa kwa hamu ya “Swish” na kuamua kuipa jina la “Waves”.

Kanye West (1)

Kanye ameanika mabadiliko hayo kwenye mtandao wa twitter jana Jumanne, Januari 26, ikiwa ni siku mbili tu baada ya kuahia orodha ya nyimbo zote zitakazokuwemo kwenye albamu hiyo.

Hii itakuwa ni mara ya tatu kwa Kanye kuibadili jina albamu yake hiyo mpya ambapo mwanzoni aliita jina la So Help Me God baadaye akaibadili na kuiita Swish kabla ya hapo jana kupa tena jina lingine Waves.

“Hii sio albamu ya mwaka. Ni albamu ya maisha” aliandika Kanye.

Travis Scott, ambaye pia ataonekana kwenye albamu hiyo naye aliandika maneno ya kuikubali kazi hiyo na kupokea mabadiliko anayoyafanya Kanye kwenye albamu yake hiyo.

Taito ya Waves inatokana na moja ya wimbo kati ya nyimbo kumi zilizomo kwenye albamu hiyo ambayo pia ina nyimbo kama “Real Friends” na “No More Parties in LA” aliyomshirikisha Kendrick Lamar.

Orodha mpya ya nyimbo zilizomo kwenye Waves.

Leave A Reply