The House of Favourite Newspapers

Kanye West Akwama Kuwania Urais Marekani

0

NYOTA wa muziki wa hip-hop nchini Marekani, Kanye West, ameshindwa kufuzu kuwa mmoja kati ya wagombea wa urais katika mji wa Wisconsin kutokana na kuchelewa kuwasilisha nyaraka zake kwa wakati.

 

Maamuzi hayo yalifanywa na Jaji wa Mahakama ya Brown County Circuit, John Zakowski, ambapo alimwondoa msanii huyo kwenye Tume ya Uchaguzi ya Wisconsin.

 

Msanii huyo alitakiwa kupeleka nyaraka hizo kabla ya Agosti 4 saa 11 jioni, lakini yeye alifika kwenye ofisi hizo saa 11 na sekunde 14, wakati huo tayari mfumo wa upokeaji nyaraka ulikuwa umemalizika.

 

Hata hivyo,  alikata rufaa, lakini Ijumaa wiki iliopita  rufaa yake ilisikilizwa ila bado iligonga mwamba. Kanye  anaamini mwisho wa kuwasilisha nyaraka hizo ilitakiwa kuwa saa 11:01 na si kamili.

 

Leave A Reply