The House of Favourite Newspapers

Kanye West Ataki Kumuona Kim Kardashian Kwenye Mavazi Ya Utupu

MWANAMITINDO kim kardashian ameanza kupata wakati mgumu kidogo maana mume wake Kanye West ameanza kushikiria vizuri sheria za wokovu kwa kumwambia ukweli mkewe kupunguza kuvaa mavazi ya kuonesha maungo yake.

Kupitia Show ya Yahoo Entertainment ikiwa ndani ya Keeping Up With Kardashian, tuliweza kuona vazi matata alilovaa Kim kwenye Met Gala yake, ila drama zilianza usiku wa kuamkia siku ya Met Gala.

Kanye West alidai kuwa hataki kumuona mkewe akiwa kama wanawake wengine wanaoshoot nae video. Haya ndio majibu ya Kim kwa Kanye

“Wewe umenitengeneza kuwa hivi, kuwa Sexy na kujiamini, na mambo yote haya. Kama wewe upo kwenye safari yako mpya na upo kwenye mabadiliko, haimaanishi na mimi niwe pamoja na ww”, alisema Kim

Mashabiki walimuunga mkono bibie kwa asilimia zote.

 

Comments are closed.