The House of Favourite Newspapers

Kapili ajitosa umeya wa Ilala

0

IMG-20151122-WA0004Msanii  kutoka Bongo Movie Boniventure Mphuru ‘Kapili’.

MSANII kutoka Bongo Movie aliyejiingiza kwenye siasa na kuwa Diwani wa Kata ya Pugu, Boniventure Mphuru ‘Kapili’ ameweka wazi kuwa amejitosa rasmi kuwania umeya wa Ilala.

Akizungumza na kona ya Bongo Movies Kapili aliyewahi kubamba na Filamu ya Safari alisema kuwa amedhamiria kabisa kurithi nafasi ya aliyekuwa Meya wa Ilala, Jerry Silaa.

“Kwa upande wa sanaa bado naipenda ipo moyoni mwangu na siwezi kuiacha kabisa japo kwa sasa nahudumia wananchi wangu, licha ya kuwa diwani sasa hivi nataka nirithi nafasi ya Silaa (Jerry) Ilala,” alisema Kapili.

Leave A Reply